TENNIS-MICHEZO

Novak Djokovic ataka wanaume walipwe fedha nyingi

Novak Djokovic mchezaji nambari moja wa mchezo wa Tennes
Novak Djokovic mchezaji nambari moja wa mchezo wa Tennes Reuters

Mchezaji bora wa mchezo wa Tennis kwa upande wa wanaume, Mserbia Novak Djokovic anasema wachezaji wa Kiume wanastahili kulipwa fedha nyingi kuwashinda wale wa kike.

Matangazo ya kibiashara

Djokovic ametoa hoja yake akisema wakati wa michezo mbalimbali ya Kimataifa, wanaume wanapocheza huwa kuna watu wengi sana wanokuja kushuhudia michuano hiyo.

Dkojovic ametoa kauli hii baada ya kuibuka bingwa katiia mashindano ya Paribas Open nchini India.

Kwa kawaida katika mashindano makubwa kama Australian Open, US Open, French Open na Wimbledon wachezaji wa kiume na kike anayepata ushindi hulipwa kiwango sawa cha fedha.

Hata hviyo, Serena William mchezaji bora duniani kwa upande wa wanawake amekosoa kauli hiyo ya Djokoviich na kusema ni kosa kubwa.