AFCON 2017-GABON-SOKA

AFCON 2017: Congo yapiga hatua nzuri baada ya kutoka sare na Zambia

Timu ya taifa ya Congo (Mashetani Wekundu) wakati wa michuano ya AFCON 2015.
Timu ya taifa ya Congo (Mashetani Wekundu) wakati wa michuano ya AFCON 2015. KHALED DESOUKI / AFP

Safari ya mataifa ya Afrika kufuzu katika michuano ya Afrika mwaka 2017 itakayochezwa nchini Gabon, ilianza Jumatano hii, Machi 23.

Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Congo-Brazzaville imefanya vizuri kwa kwa kwenda sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya taifa ya Zambia Jumatano, Machi 23, 2016. Matokeo haya yanaiweka Congo-Brazzaville katika nafasi nzuri katika kundi E, wakati ambapo Kenya, ikiwa ugenini, wameangukia pua kwa kufungwa na Guinea-Bissau bao 1-0.

Zambia walikuwa wakiongoza 1-0 baada ya mchezaji Kalengo kuingiza mpira wavuni katika dakika ya 60, lakini hadi kipenga cha mwisho walijikuta wanakwenda sare na Congo-Brazzavile ya kufungana bao 1-1 baada ya Massengo kusawazisha katika dakika ya 75 ya mchezo.

Wakati huo huo timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wamejiandikishia alama tatu baada ya kuimenya timu ya taifa ya Chad bao 1-0.

Hayo yakijiri Beni wmeshindwa kufanya vizuri na kujikuta hadi dakika ya mwisho ya mchezo wkifungwa na sudani Kusini mabao 2-1.

Mechi zingine zitakazopigwa Alhamisi hii, Machi 24:

Comoros vs Botswana

Djibuti vs Liberia

Ghana vs Msumbiji

Madagascar vs Jamhuri ya Afrika ya Kati

Hii ni michuano ya makundi kati ya mataifa mbalimbali na michuano ya marudiano itachezwa wiki ijayo.