UHOLANZI-JOHAN CRUYFF-SOKA

Shujaa wa soka wa Uholanzi, Johan Cruyff, afariki

Mholanzi Johan Cruyff katika mechi ya Kombe la Dunia mwaka 1974 dhidi ya Argentine.
Mholanzi Johan Cruyff katika mechi ya Kombe la Dunia mwaka 1974 dhidi ya Argentine. STF / AFP

Kifo cha Johan Cruyff, aliefariki katika mji wa Barcelona Machi 24 kutokana na kansa kimezua hisia mbalimbali ulimwenguni. Johan Cruyff alikuwa shujaa wa jumla wa soka katika miaka ya 1970. Kisha alianzisha mtindo wa Barca, ambayo imekua sasa kumbukumbu katika ulimwengu wa soka.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutangazwa kifo cha Johan Cruyff, hisia mbalimbali zimeendelea kutolewa. ulimwengu wa soka kwa kauli moja unamchukulia Johan Cruyff kama mtu aliefanya maajabu katika mpira wa miguu. "Alikuwa mchezaji bora wa miaka yote," Michel Platini amesema baada ya kutangazwa kwa kifo cha shujaa huyo wa soka. Platini aliyepata mara tatu tuzo ya mpira wa dhahabu (Golden Ball), anasema kwamba "dunia imepoteza mtu muhimu."

"Nilipatwa na msisimuko na nilipigwa na butwaa kusikia taarifa hiyo yenye huzuni, kwani sikutarajia sasa hivi, hata kama tulikua na taarifa kuwa anakabiliwa na saratani, kipa wa zamani wa Cameroon, Joseph-Antoine Bell, amesema. Kwa hakika alikuwa mmoja kati ya wachezaji wawili au watatu bora ambo historia ilifahamu. Baada ya Pelé, alionyesha kwamba katika kila kizazi kunaweza kupatikan mchezaji bora. "

Kocha Claude Le Roy, ambaye ana umri sawa na Johan Cruyff (miaka 68), anakaribisha ushawishi muhimu wa raia huyo wa Uholanzi: "Alikuwa na mtindo wa aina yake ambao nakubali kama kocha. Pia aliwahi kunihudumia vizuri wakati nilikuwa mchezaji wa kimataifa. Kipaji chake kilikua hakina mpinzani. "

Franz Beckenbauer amesema kuwa "ameshtushwa" kwa kifo cha "ndugu" yake.

Luis Figo raia wa Ureno, aliyekuwa kiungo wa FC Barcelona na Real Madrid hasa, ambaye alipata tuzo ya mpira wa dhahabu (Golden Ball) mwaka 2000, ametumia mtandao wa Twitter kueleza hisa zake: "Alikuwa kocha wangu wa kwanza nje ya nchi, mmoja wa makocha wangu ambao sijawahi kuwapata. Mtu muhimu sana katika kazi yangu. Ni hasara kubwa. " "Tunamkosa shujaa mwingine," Lionel Messi amesma. "Hatutokusahaukamwe," ameandika Diego Maradona, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina.

Kwenye runinga ya Barça ( Barça TV), Andrés Iniesta, mchezaji wa Uhispania, ambaye ni nahodha wa FC Barcelona anasema kwamba "hii ni siku ya huzuni sana, si tu kwa familia ya Barça lakini kwa soka duniani" na "kwa wale wote ambao waliona ushawishi aliokuwa nao mtu wa namna hii katika soka. "

AFP