AFCON 2017-KENYA-GUINEA-SOKA

Mchuano kati ya Kenya na Guinea Bissau kukumbwa na fujo

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars.
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars. youtube

Fujo za mashabiki katika uwanja wa soka wa Nyayo jijini Nairobi nchini Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita kati ya wenyeji Harambee Stars na Guinea Bissau zilisababisha mchuano wa kutafuta tiketi ya kufuzu kwa fainali za michuano ya Afrika kusimamishwa kwa zaidi ya dakika 30.

Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo ilianza kushuhudiwa katika dakika 83 baada ya Guinea Bissau kupata bao ambalo wachezaji na mashabiki wa Kenya walidai kuwa haukuwa umevuka mstari baada ya kuguswa na kipa Arnold Origi.

Kenya ambayo pia ilifungwa na Guinea Bisssau bao 1 kwa 0 ugenini mjini Bissau na kwa matokeo hayo matumaini ya Kenya ya kufuzu katika michuano hiyo yamefifia kabisa.

Kundi hili linaongozwa na Guinea-Bissau ambayo ina alama 7, mbele ya Congo Brazaville ambayo ina alama 6 sawa na Zambia huku Kenya ikiwa na alama 1. Zambia na Congo Brazavile zilitoka sare ya bao 1 kwa 1.

Matokeo mengine ya Jumapili iliyopita, Ghana ilishindwa kupata ushindi baada ya kutoka sare ya ya kutofugana na Msumbiji jijini Maputo.

Black Stars inaongoza kundi H kwa alama 10, Mauritius ni ya pili kwa alama 6 na ikiwa itashinda siku ya Jumanne dhidi ya Rwanda jijini Kigali bali itaikaribia Ghana.

Matokeo mengine, Benin wakicheza nyumbani waliwafunga Sudan Kusini mabao 4 kwa 1 huku Bostwana ikiwalemea Comoros kwa mabao 2 kwa .

Katika hatua nyingine, Kutoka na timu ya Chad kujitoa katika michuano hii Shirikisho la soka barani Afrika CAF limepigwa faina ya Dola elfu 20,000 na kufungiwa kutokushiriki michuano ya Afcon kwa mwaka mmoja.

Chad ambayo ilikuwa katika kundi moja la G na Misri, Nigeria na Tanzania ilijiondoa katika dakika za lala salama wakati ikitarajiwa kufika Dar es salaam kwa mchunao wa marudiano siku ya Jumatatu, kwa madai kuwa haikuwa na fedha za kuendelea kushiriki katika michuano hiyo.

Hii inaamana kuwa matokeo ya mchuano dhidi ya Chad yamefutwa na sasa zinasalia timu tatu. Misri inanendelea kuwa kileleni kwa alama 4 ikifuatwa na Nigeria ambayo ina alama 2 huku Tanzania ikiwa ya mwisho kwa alama 1.
Mchezo ujao wa Tanzani utakuwa ni mwezi Juni jijini Dar es salaam dhidi ya Misri.

Michuano ya Jumatatu Machi 28, 2016

Zimbabwe vs Swaziland
Jamhuri ya afrika ya Kati vs Madagascar
Libya vs Sao Tome e Principe
Equitorial Guinea vs Mali
Sierra Leone vs Gabon

Jumanne Machi 29, 2016

Malawi vs Guinea

Lesotho vs Seychelles

Rwanda vs Mauritius

Ethiopia vs Algeria

Niger vs Senegal

Namibia vs Burundi

Togo vs Tunisia

Angola vs D.R. Congo

Liberia vs Djibouti

Uganda vs Burkina Faso

Gambia vs Mauritania

Egypt vs Nigeria

Afrika Kusini vs Cameroon

Sudan vs Cote d'Ivoire

Morocco vs Cape Verde