AFCON 2017-DRC-ANGOLA-SOKA

AFCON 2017: DRC yapata ushindi Angola

CAF

Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imerudi kuwa kileleni katika Kundi B baada ya kupata ushindi mjini Luanda dhidi ya Angola kwa mabao 2-0. Mabao ambayo yaliwekwa kimyani na wachezaji wawili wa klabu ya TP Mazembe.

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa na alama 9, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo sasa iko mbele ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo ni ya pili ikiwa na alama 7.

Timu ya taifa ya DR Congo imefanikiwa kupata ushindi dhidi ya Angola na kuchukua na fasi ya kwanza katika kundi B, baaada ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kuiadhibu Madagascar Jumatatu wiki hii na kupata ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchuano wa awali Timu ya taifa ya Angola (Palancas Negras), ilifungwa na DR Congo kwa mabao 2-1mjini Kinshasa siku nne zilizopita. Huu ni ushindi muhimu kwa timu ya taifa ya DR Congo.

Baada kuvumilia mashambulizi ya Angola katika dakika za mwanzo za mchezo, huo, wachezaji wa kocha Florent Ibenge walipachika bao la kwanza katika dakika za lala salama za kipindi cha kwanza cha mchezo, kabla ya mapumziko kupitia beki Joël Kimwaki Mpela wa klabu ya TP Mazembe katika dakika ya 45. Bao la pili limefungwa katika dakika ya 90 na mshambuliaji, Jonathan Bolingi, pia mchezaji wa TP Mazembe.

Kufuatia ushindi huo, DR Congo wanaongoza katika Kundi B na hatimaye kuwa na hatima yao mkononi. Wengi hawakufikiria kuwa DR Congo itafikia kwenye nafasi hiyo tangu mwanzo wa michuano hiyo, hasa baada ya kushindwa mcuano wake na Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa mabao 2-1.

Vijana wa Ibenge ambao watasafiri kwenda Madagascar katika michuano itakayoendelea (Juni 3, 4, 5) wanatakiwa kujidhatiti na kutwa ushinda ugenini, kwani timu ya taifa ya Madagascar haijashindwa nyumbani katika michuano hii.