BARCELONA-ATLETICO-SOKA

Barcelona yaishinda Atletico nyumbani

Luis Suarez  amewanyamanzisha Atletico Madrid kwa mara ya pili.
Luis Suarez amewanyamanzisha Atletico Madrid kwa mara ya pili. Reuters / Albert Gea Livepic EDITORIAL USE ONLY

FC Barcelona imewaacha kinywa wazi Atletico Madrid baada ya kuwafunga mabao 2-1 katika robo fainali ya awali ya Ligi ya Mabingwa wa soka Jumatano hii Aprili 5, 2016 katika uwanja Camp Nou mjini wa Catalonia.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo haya, hata hivyo, yanawapelekea Atletico Madrid kuwa na bahati ya kufuzu katika nusu fainali, katika mechi ya marudiano ya tarehe 13 Aprili.

Timu ya Barcelona imeanza vizuri mchezo wake wa kwanza ya hatua ya robo fainali ya klabu bingwa ulaya.

Mshambuliaji Luis Suarez ndie alifunga mabao yote mawili. Bao la kwanza ambalo ni la kusawazisha, lilifungwa katika dakika ya 63. Na bao la pili ambalo ni la ushindi, lilifungwa katika dakika 74.

Bao la Atletico Madrid lilifungwa na Fernando Torres katika dakika ya 25. Hata hivyo Torres alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili za njano.

Katika mchuano mwingine Bayern Munich wakiwa ugenini na wenyeji wa Benfica wamepata ushindi wa bao 1-0. Bao la Bayern Munich liliwekwa kimyani na Arturo Vidal.