UEAFA-SOKA

Liverpool watoka sare na Borrusia Dortmund

Wachezaji wa Liverpool wakifurahia ushindi wao dhidi ya Cardiff.
Wachezaji wa Liverpool wakifurahia ushindi wao dhidi ya Cardiff.

Alhamisi hii usiku Liverpool wamemenyana na wenyeji wake Borrusia Dortmund, hadi kipenga cha mwisho, timu hizi mbili zilijikuta zikitoka sare ya kufungana bao 1-1.

Matangazo ya kibiashara

Bao la Liverpool lilifungwa na kiungo Divock Origi. Bao la kusawazisha kwa upande wa Borrusia Dortmund, lilifungwa na beki wa timu hiyo Mats Hummels.

Kwa siku ya jana pekee michezo minne ilipigwa katika katika viwanja mbalimbali.

Sparta Prague wakiwapokea Villarreal walikubali kichapo cha mabao 2-1 katika uwanja wa El Madrigal. Cedric Bakambu ambaye alionekana nyota katikka mchuano huo ndiye alifunga mabao yote mawili. Balo la kufutia machozi la Sparta Prague lilifungwa na Jakub Brabec.

Shakhtar Donetsk wakiwa ugenini waliifunga Sporting Braga mabao 2-1. Mabao ya Shakhtar Donetsk yaliwekwa kimyani na wachezaji Yaloslav Rakitskiy na Facundo Ferreyra. Naval Costa Eduardo ndiye aliifungia klabu yake ya Sporting Braga bao la kufutia machozi.

Katika mechi nyingine Sevilla waliwaburuza Athletic Bilbao kwa mabao 2-1. Mabao ya Sevilla yalifungwa na Timothee Kolodziejczak na Vicente Iborra. Bao la Athletic Bilbao lilifungwa na Aduriz Zubeldia.