UEFA-SOKA

Bayern Munich yafanikiwa kutinga nusu fainali

Bayern Munich watinga nusu fainali baada ya kuibandua Benfica katika Jumatano usiku Aprili 13, 2016..
Bayern Munich watinga nusu fainali baada ya kuibandua Benfica katika Jumatano usiku Aprili 13, 2016.. Reuters / John Sibley Livepic

Bayern Munich imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Benfica, katika mechi ya marudiano iliyopigwa Jumatao hii usiku.

Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo mwingine Barcelona ilivuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuburuzwa kwa mabao 2-0 na Atletico Madrid. Mabao yote ya Altletico Madrid yalifungwa na Antoine Griez-mann. Bao la pili la klabu hiyo lilifungwa kwa njia ya penalti.

Mabao ya Benfica yalifungwa na Raul Alonso Rodriguez na Anderson Souza Conceicao, huku mabao ya Bayern Munich yakifungwa na Arturo Vidal na Thomas Muller.

Kwa hiyo Benfica na Barcelona zimebaduliwa katika michuano hii, huku klabu za Bayern Munich na Atletico Madrid zikitinga nusu fainali.

Katika mechi ya awali iliyopigwa katika uwanja wa Camp Nou, Atletico Madrid walifungwa 2-1, lakini katika mchuano wa marudiano klabu hii ilifanya vizuri kwa kupata ushindi wa mabao 2-0, na hivo kujikatia tiketi ya kutinga nusu fainali.

Bayern Munich na Atletico Madrid wanaungana na Manchester City pamoja na Real Madrid katika nusu fainali. Droo ya nusu fainali itapangwa Ijumaa wiki hii.