UEFA-SOKA

Timu 4 zatinga nusu fainali

Mshambuliaji wa Sevilla FC, Kevin Gameiro (katikati), aliyekamilisha ushindi wa timu yake dhidi ya Athletic Bilbao, Aprili 14, 2016 katika uwanja wa Sanchez Pizjuan.
Mshambuliaji wa Sevilla FC, Kevin Gameiro (katikati), aliyekamilisha ushindi wa timu yake dhidi ya Athletic Bilbao, Aprili 14, 2016 katika uwanja wa Sanchez Pizjuan. AFP

Hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepigwa Alhamisi hii, Aprili 14 kwa michezo minne.

Matangazo ya kibiashara

Sevilla imeiondoa Athletic Bilbao kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi ya awali na ya maurudiano timu zote mbili kujikuta zimetoka sare ya kufungana jumla ya mabao 3-3 baada ya kila timu kushinda 2-1 mechi ya nyumbani.

Villarreal imeinyeshea mvua ya mabao Sparta Praga kwa kuichapa 4-2, huku Liverpool ikiilamba Borrussia Dortmund mabao 4-3.

Magoli ya Liverpool yamewekwa wavuni na Divock Origi, Philippe Coutinho, Mamadou Sakho na Dejan Lovren.

Kwa upande wa Dortmund, wachezaji Henrikh Mkhitaryan, Pierre-Emerick Aubameyang na Marco Reus waliliona lango la Liverpool.

Sevilla, Villarreal, Liverpool na Shakhtar Donetsk wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Ulaya.