NIGERIA, NFF-SOKA

Ibrahim Galadima, kiongozi wa kamati ya maridhiano ya NFF

Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Nigeria wakati wa Kombe la Dunia 2015.
Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Nigeria wakati wa Kombe la Dunia 2015. Rich Lam / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP

Rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Nigeria Ibrahim Galadima ameteuliwa kuongoza kamati ya maridhiano kusaidia kutatua mzozo wa viongozi wa soka katika Shirikisho hilo.

Matangazo ya kibiashara

Bwana Galadima ambaye amewahi kuwa rais wa NFF kati ya mwaka 2002 na 2006, ameteuliwa na Waziri wa Michezo Solomon Dalung ambaye amasema anataka kuona amani katika Shirikisho hilo.

Kwa kipindi kirefu sasa Chris Giwa ameendelea kupinga uongozi wa rais wa NFF anayetambuliwa na FIFA Amaju Pinnick.

Hivi karibuni Mahakama iliamua kuwa Giwa anastahili kuongoza soka nchini humo na tayari Shirikisho la soka FIFA imetishia kuifungia Nigeria ikiwa itaendelea kuingilia maswala ya soka nchini humo.