KENYA LEOPARS-SOKA
AFC Leopards mbioni kuwakosa wachezaji wake 10
Imechapishwa:
Mabingwa wa zamani wa soka ligi kuu nchini Kenya AFC Leopards wanapanga kuachana na wachezaji 10 wakati wa kipindi cha dirisha dogo la kuwasajili wachezaji mwezi ujao.
Matangazo ya kibiashara
Kocha Ivan Minnaert anatarajiwa kutumia nafasi hiyo kuwatafuta wachezaji watakaoisadia klabu hiyo kunyakua ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
Miongoni mwa wachezaji wanatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ni pamoja na mabeki Israel Emuge, Erick Masika na Solomon Nasio.
AFC Leopards ambayo mwisho ilishinda taji kuu la ligi kuu nchini Kenya mwaka 1998 ni ya tano kwa alama 18.