ATLETICO-BAYERN-SOKA

Ligi ya Mabingwa: Atletico pia yailamba Bayern Munich

Antoine Griezmann akishrehekea bao lake dhidi ya Bayern Munich Mei 3 2016.
Antoine Griezmann akishrehekea bao lake dhidi ya Bayern Munich Mei 3 2016. Reuters / Michaela Rehle

Bayern Munich walikua na matumaini madogo ya kupata ushindi katika fainali ya michunao ya Ligi ya Mabingwa baada ya kupoteza katika mechi ya awali (0-1).

Matangazo ya kibiashara

Licha ya mabao mawili yaliyofungwa na Xabi Alonso na Robert Lewandowski, Wajerumani walijikuta wamesalimu amri baada Mfaransa Antoine Griezmann kupunguza matokeo kwa kufuinga timu yake bao moja (2-1). Timu zote mbili zilikosa penalti.

Jumanne hii jioni, Bayern Munich walikua na wazo moja tu, la kuvunja ukuta wa Atletico Madrid. Msimu huu, Atletico Madrid wamefungwa mabao matano tu tangu kuanza kwa michuano. Kutokana na timu hii kutoacha kusonga mbele, Wajerumani na Pep Guardiola, mtume kwa kutawala mpira, wangeliweza kupata ufumbuzi baada ya kucharazwa 1-0 katika mchuano wa awali kwa kuwa kwanza na hatua moja mbele.

Thomas Müller ashindwa penalti!

Pamoja na Bayern Munich kutawala mpira katika mchunao wake dhidi ya Atletico Madrid, lango la Kislovenia Jan Oblak halikuweza kushambuliwa katika kipindi cha kwanza. Hata hivyo Robert Lewandowski alionyesha ubabe wake katika dakika ya 20 na katika dakika ya 23 kwa kujitahidi kulishambulia lango hilo bila mafanikio. Lakini Jan Oblak anaonekana kiungo muhimu kwa timu hii ya Atletico. Mfaransa Antoine Griezmann ambaye aliweza kuikunja Barca katika robo fainali alionekana mchezaji bora kabisa katika mchuano wa Jumanne jioni.

Hata hivyo katika dakika ya 35 Thomas Müller alishindwa kufanya vizuri baada ya Bayern kupata penalti.

Hakuna Ligi ya Mabingwa kwa Pep Guardiola

Katika kipindi cha pili Atletoco Madrid walikuja juu, na katika dakika ya 54, mfaransa Griezmann alibahatika kuliona lango la Bayer Munich na kupunguza matokeo ya awali (2-1).

Dakika chache tu kabla ya kipenga cha mwisho, Atletico Madrid, ambao walikua na matumani ya kupata ushindi, ilishindwa penalti. Hata hivyo Bayern walikua bado wana matumaini ya kufanya vizuri, lakini Atletico waliendelea kujidhatiti hadi mwisho wa mchuano huo. Pep Guardiola ataondoka klabu hii bora ya Ujerumani bila hata hivyo kunyakua Kombe.