NIGERIA_-YEKINI-SOKA
Miaka minne toka nyota wa Super Eagles afariki
Imechapishwa:
Wapenzi wa soka nchini Nigeria, na kwingineko barani Afrika leo hii wanamkumbuka Rashidi Yekini mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Super Eagles aliyefariki dunia siku kama ya leo mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 48.
Matangazo ya kibiashara
Mshambuliaji huyo atakumbukwa kwa muda mrefu kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa Nigeria kuwahi kufunga goli wakati wa michuano ya kombe la duniani mwaka 1994 ilipoandaliwa nchini Marekani na Nigeria kushiriki kwa mara ya kwanza na kushinda Bulgaria mabao 3 kwa 0.
Pamoja na kuichezea Super Eagles Yekini aliwahi pia kuvchezea vlabu mbalimbali nchini Uhispania, Ugiriki, Ureno na Uswisi.