Real Madrid kumenyana na Manchester City
Imechapishwa:
Klabu ya Real Madrid nchini Uhispania umatano hii usiku watakuwa wenyeji wa Manchester City ya Uingereza katika mchuano wa marudiano wa nusu fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya.
Mchuano wa kwanza katika uwanja wa Etihad, vlabu hivi vilitoka sare ya kutofungana.
Swali ambalo mashabiki wa Manchester City wanajiuliza je, watafuzu katika hatua ya fainali na kuweka historia ya kucheza katika fainali ya UEFA ?
Real Madrid inayofunzwa na Zinadine Zidane watamkosa Kiungo wa kati Casemiro na mshambuliaji Karim Benzema huku kocha wa Manchester City Manuel Pelegrini anakabiliwa na kibarua cha kumtafuta atakayechukua nafasi ya kiungo wa kati David Silva.
Mechi hii itaanza saa tatu na dakika 45 saa za Afrika Mashariki na mshindi atakutana na Atletico Madrid ya Uhispiania iliyofuzu jana Jumanne.
Fainali itachezwa tarehe 28 mwezi huu katika uwanja wa San Siro mjini Milan nchini Italia.