CAMEROON-SOKA

Cameroon yampoteza Jeanine Christelle Djomnang

Jeanine Christelle Djomnang.
Jeanine Christelle Djomnang. Fécafoot

Baada ya kifo cha mchezaji wa Cameroon Patrick Ekeng siku tatu zilizopita wakati wa mechi ya ligi kuu ya Romania, Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT) imetangaza Mei 8 kifo cha kipa Jeanine Christelle Djomnang.

Matangazo ya kibiashara

Hili ni pigo kubwa kwa soka nchini Cameroon. Chini ya masaa 48 baada ya kifo cha ghafla cha kiungo Patrick Ekeng dakika saba baada ya kuingia uwanjani wakati wa mechi ya ligi kuu ya Romania, Jumapili Mei 8, Shirikisho la Soka la Cameroon lilitoa taarifa ya kuhuzunisha ya kifo cha kipa Jeanine Christelle Djomnang.

Mwanamkehuyo mwenye umri wa miaka 26 angelishiriki katika mechi ya mzunguko wa 6 ya michuano ya wanawake ya daraja la kwanza nchini Cameroon kati ya timu yake, Femina Stars ya Ebolowa na Louves Minproff. Kwa mujibu wa afisa wa mawasiliano wa FECAFOOT, Laurence Fotso, Jeanine Christelle Djomnang alidondoka dakika chache kabla ya mchuano huo kutimua vumbi wakati ambapo alikua akipata mazoezi na wachezaji wenzake katika uwanja wa ,pira wa manispa ya jiji la Ebolowa kusini mwa Cameroon.

Taarifa ya kifo cha mwanamke huyo ilijulikana dakika chache baadaye, sababu za kifo hicho mpaka sasa hazijajulikana. FECAFOOT inasema kwa sasa inasubiri ripoti rasmi ili kuweka wazi mazingira halisi ya kifo cha Jeanine Christelle Djomnang.