RWANDA-SOKA

Ligi kuu Rwanda: APR na Rayon Sport wafukuzana

Uwanja wa mpira wa Amahoro mjini Kigali, moja ya viwanja kunako chezwa ligi kuu ya Rwanda.
Uwanja wa mpira wa Amahoro mjini Kigali, moja ya viwanja kunako chezwa ligi kuu ya Rwanda. AFP

Vlabu vya Rayon Sport na APR vinaendelea kufukuzana kuwania ubingwa wa ligi kuu ya soka msimu huu baada ya APR kucheza mechi 22 na Rayon Sport mechi 21.

Matangazo ya kibiashara

APR FC inaongoza kwa alama 49 huku Rayon ikiwa ya pili kwa alama 48. Mukura FC ni ya tatu kwa alama 41.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rayon Sports ilipata ushindi mnono wa mabao 4 kwa 0 dhidi ya Rwamagana City.

APR nayo ilitoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Sunrise FC.

Matokeo mengine ya mwishoni mwa juma:

  • Gicumbi Fc 0-3 Police FC
  • Etincelles Fc 2-0 SC Kiyovu
  • AS Muhanga 1-3 Mukura (Inashikilia nafasi ya tatu kwa alama 41.
  • AS Kigali nayo imepanda hadi katika nafasi ya nne, kwa alama 40 baada ya kuishinda Espoir FC mabao 2 kwa 0.

Ligi kuu ya Rwanda ina timu 16 na mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini humo ambao katika historia wameshinda mara 14.

Hii ni klabu ya jeshi na pia imekuwa ikishriki katika mashindano ya barani Afrika na mwaka 2004, ilifanya vizuri kwa kufika katika hatua ya pili na kuondolewa na klabu ya Afrika Sports National ya Cote d'Ivoire.

Imeshinda taji la CECAFA mara tatu mwaka 2004, 2007 na 2010.

Mara ya mwisho kwa Rayon Sports kushinda taji hili ilikuwa ni mwaka 2013 na imeshinda taji hili mara 7 lakini imewahi kunyakua taji la CECAFA mwaka 1998 na pia kushiriki katika michuano ya klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika.

Ratiba ya Jumanne Mei 10, 2016

  • Bugesera Fc vs Rayon Sports (Nyamata)
  • Musanze Fc vs Marines Fc (Nyakinama)
  • Rwamagana City FC vs Sunrise FC (Rwamagana )
  • APR Fc vs Gicumbi Fc (Stade de Kigali)