ETHIOPIA-SOKA

Haile kocha mpya wa timu ya taifa ya Ethiopia

Adane Girma, aliyefunga bao la kusawazisha, alikua mtu muhimu wa mechi ya Ethiopia dhidi ya Zambia
Adane Girma, aliyefunga bao la kusawazisha, alikua mtu muhimu wa mechi ya Ethiopia dhidi ya Zambia REUTERS/Thomas Mukoya

Shirikisho la soka nchini Ethiopia limemteau Gebremedhin Haile kuwa kocha mpya wa timu ya taifa.

Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo wa klabu ya Defence FC, ataiongoza timu ya taifa katika michuano miwili ya kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika AFCON nchini Gabon mwaka ujao dhidi ya Lesotho na Ushelisheli.

Mapema mwezi huu, EFF ilimfuta kazi kocha Yohannis Sahle kwa sababu ya matokeo mabaya katika michuano ya kufuzu kucheza fainali za Afrika.

Wakati akiifunza timu ya taifa, Sahle aliiongoza Walia Ibex hadi katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA mwaka uliopita, lakini pia michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN iliyofanyika nchini Rwanda mapema mwaka huu.