MAN UTD-BOURNEMOUTH-SOKA

Bomu feki lazua kizaaza Old Trafford

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson katika uwanja wa Old Trafford.
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson katika uwanja wa Old Trafford. REUTERS/Phil Noble

Watazamaji 75600 walitakiwa kuondoka Jumapili hii iliyopita katika uwanja wa Old Trafford, wakati walipokua wakijiandaa kutazama mchuano kati ya Machester United na Bournemouth.

Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo ulichukuliwa na polisi baada ya kugundua kifaa kilichofananishwa na bomu. Mara moja mchuano ulikua unatazamiwa klupigwa ulifutwa na kuahirishwa hadi Jumanne Mei 17 2;00 usiku.

Kifaa hicho kiliachwa katika uwanja huo na kampuni moja ya ulinzi iliyokuwa ikifanya mazoezi na mbwa wa kunusa vilipuzi siku nne zilizopita. Ugunduzi huo ulisababisha mechi ya mwisho ya ligi kuu msimu huu katika uwanja huo wa Manchester United kuahirishwa na mashabiki kuamriwa kuondoka.

Polisi jiji la Manchester katika akaunti yake ya Twitter immesema kuwa kifaa kilichopatikana katika uwanja wa Old Trafford, hakikuwa bomu bali kilikuwa kifaa cha mafunzo ya vilipuzi.