RWANDA-SOKA

Ernest Sugira awasili Kinshasa

Timu ya taifa ya Rwanda, Novemba 2015.
Timu ya taifa ya Rwanda, Novemba 2015. AFP PHOTO / SALAH LAHBIBI

Mshambuliaji wa klabu ya AS Kigali nchini Rwanda Ernest Sugira amewasili jijini Kinshasa kufanya mazungumzo ya klabu ya AS Vita Club.

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa wa soka nchini DRC wamesema watatumia Dola za Marekani Dola 130,000 kumsajili mchezaji huyo wa Rwanda ambaye atakuwa ghali sana kuwahi kusajiliwa kwa kiasi hicho cha fedha.

Kocha Florent Ibenge alikuwa katika uwanja wa ndege kumpokea mchezaji huyo wa kimaifa kutoka Rwanda mwenye umri wa miaka 24.

Ikiwa mambo yatakwenda vizuri, atashiriki katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.