TENNIS-MICHEZO

Maclagan: “ Murray yuko tayari kushiriki French Open”

mchezaji wa Tennis Andy Murray kutoka Uingereza.
mchezaji wa Tennis Andy Murray kutoka Uingereza. Geoff Burke-USA TODAY

Miles Maclagan kocha wa zamani wa mchezaji wa Tennis Andy Murray kutoka Uingereza anasema mchezaji huyo yuko katika hali nzuri kuelekea mashindano ya French Open yanayoanza tarehe 22 mwezi huu.

Matangazo ya kibiashara

Murray ambaye anashikilia nafasi ya pili duniani, siku ya Jumapili alimshinda Novak Djokovich bingwa wa dunia katika fainali ya Italian Open.

Mwaka uliopita, Murray alifika katika hatua ya nusu fainali katika mashindano ya French Open.