UINGEREZA-SOKA

Roy Hodgson akitaja kikosi cha wachezaji wake

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson ambaye leo ametangaza kikosi chake
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson ambaye leo ametangaza kikosi chake thefa.com

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uingereza Roy Hodgson amekitaja kikosi cha wachezaji 26 kuanza maandalizi ya kushiriki michuano ya mataifa bingwa barani Ulaya, nchini Ufaransa kuanzia tarehe 10 mwezi ujao hadi tarehe 10 Julai.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wachezaji waliotajwa ni pamoja na Marcus Rashford mchezaji wa Manchester United mwenye umri wa miaka 18, Andros Townsend wa Newcastle na Jack Wilshere miongoni mwa wengine.

Lakini kocha Hodgson amewaacha wachezaji wengine kama Theo Walcott, Phil Jagielka, Jermain Defoe na Mark Noble.

Mataifa 24 barani Ulaya yatashiriki katika michuano hiyo na yana hadi tarehe tarehe 31 mwezi Mei kuwasilisha majina ya mwisho ya wachezaji 23 kushiriki katika mashindano hayo.