UHISPANIA-SOKA

Vicente del Bosque akitaja kikosi chake cha wachezaji

Vicente del Bosque kocha wa timu ya taifa ya Uhispania.
Vicente del Bosque kocha wa timu ya taifa ya Uhispania. Reuters

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uhispania Vicente del Bosque, amekitaja kikosi cha wachezaji 25 kuanza maandalizi ya michuano ya mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa kuanzia mwezi ujao.

Matangazo ya kibiashara

Del Bosque amesema kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 atakitaja mwisho wa mwezi huu.

Kocha huyo ameshangaza wengi kwa kuwaacha wachezaji wenye majina makubwa kama Fernando Torres, Juna Mata, Diego Costa na Javi Martinez.

Mchezaji wa Arsenal Santi Cazorla pia ameachwa kwa sababu ya jeraha la goti.

Kocha Del Bosque ameonekana kuwapa nafasi wachezaji chipukizi kushiriki katika mashindano haya.

Mbali na Uhispania, kocha wa Ujerumani Joachim Loew naye, amekitaja kikosi chake cha wachezaji 27.

Miongoni mwa wachezaji hao ni beki Jerome Boateng, Kiungo wa kati Josha Kammich, Lukas Podoski, Thomas Mulla , Mesut Ozil miongoni mwa wengine.

Kikosi cha mwisho kitatajwa tarehe 30 mwezi huu.

Nchini Uingereza, hatimaye mchuano wa kumaliza ligi kuu ya soka nchini humo kati ya Manchetser United na Buner bra, unahcezwa kuanzia saa Moja Kamili saa za Afrika Mashariki katika uwnaja wa Old Trafford.

Mchuano huu ulikuwa umeratibiwa kuchezwa mwishoni mwa juma lililopita lakin kwa hifu ya usalama uliahirishwa.