TANZANIA-SOKA

Mkwasa akitangaza kikosi chake

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania wakifanya mazoezi kabla ya mechi yao ya leo jioni
Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania wakifanya mazoezi kabla ya mechi yao ya leo jioni Kwa hisani ya Blog ya Issa Michuzi

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa amekitaja kikosi cha wachezaji 26 kuanza kujiandaa kumenyana na Harambee Stars ya Kenya katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki tarehe 29 mwezi huu jijini Nairobi.

Matangazo ya kibiashara

Taifa Stars pia itatumia mchuano huo kujiweka tayari kumenayana na Misri tarehe 4 mwezi ujao jijini Dar es salaam, huku Kenya ikijiweka tayari kucheza na Congo-Brazaville jijini Nairobi, kufuzu kucheza fainali ya Afrika nchini Gabon mwaka ujao.

Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na Beki wa Yanga Nadir Haroub alimaarufu kama Cannavaro ambaye awali alikuwa ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa.

Makipa: Deo Munish ( Yanga), Aishi Manula (Azam) Benno Kakolanya ( Prisons).

Mabeki: Juma Abdul, Haji Mwinyi,Nadir Haroub (Yanga ), Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris ( Azam), Mohamed Tshabalala (Simba), Andrew Vicent ( Mtibwa Sugar).

Viungo wa Kati: Hamid Mao, Farid Mussa ( Azam), Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya ( Mtibwa Sugar ),Hassan Kabunda ( Mwadui ), Juma Mahadhi (Coastal Union). Ismail Issa Juma ( JKU)

Washambuliaji: Elias Maguri ( Stand United), John Bocco ( Azam) Ibrahim Hajib ( Simba), Mbwana Samatta ( Genk GRC, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu ( TP Mazembe)

Naye kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uganda Milutin “Micho” Sredojovic amekitaja kikosi cha wachezaji 21 kuanza mazoezi kuikabili Zimbabwe katika mechi ya kirafiki tarehe 31 mwezi huu na baadaye kukabaliana na Bostwana katika mchuano wa kufuzu kuchgeza fainali za Afrika.

Makipa:1/Onyango Denis – Mamelodi Sundowns-SA, 2/Jamal Salim Magoola- El Merreikh-Sudan 3/Odongkara Robert- Saint George-Ethiopia

Mabeki: 4/Iguma Denis –Al Ahed-Lebanon, 5/Isinde Isaac-
Saint George-Ethiopia, 6/Jjuko Murushid- Simba SC-Tanzania, 7/Waswa Hassan- Al Shorta-Iraq ,8/Ochaya Joseph- KCCA Fc -Ugand

Viungo wa Kati: 9/Azira Mike- Colorado Rapids-USA, 10/Aucho Khalid- Gor Mahia-Kenya, 11/Mawejje Tony- Thottur-Iceland, 12/Oloya Moses-Binh Duong-Vietnam,13/Kizito Luwagga Wiliam Feirense-Portugal, 14/Walusimbi Godfrey-Gor Mahia-Kenya

Washambuliaji: 15/Miya Farouk-Standard Liege- Belgium, 16/Lorenzen Melvyn-
Werder Bremen-Germany, 17/Massa Geoffrey- Bloemfontein Celtics-SA, 18/Kasirye Davis- Rayon Sports-Rwanda, 19/Okwi Emanuel-Sondyerske-Denmark, 20/Sekisambu Erisa-Vipers -Uganda, 21/Lubega Edrisa –Proline -Uganda