SEVILLA-LIVERPOOL-SOKA

Sevilla yanyakua Kombe la Ulaya

Wachezaji wa klabu ya Uhispania ya Sevilla washerehekea ushindi wao dhidi ya Liverpool.
Wachezaji wa klabu ya Uhispania ya Sevilla washerehekea ushindi wao dhidi ya Liverpool. Reuters

Klabu ya Uhispania ya Sevilla imetwaa Kombe la Ulaya kufuatia ushindi wake dhidi ya Liverpool ya Uingereza, kwa kuwatandika mabao 3-1. Hii ni mara ya tatu mfululizo klabu ya Sevila kutwaa Kombe hili la Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Liverpool ndio walianza kuliona lango la Sevilla. Hata hivyo klabu hii ya Uingereza ilitawala na kuongoza katika kipindi cha kwanza, lakini Sevilla walisawazisha mwanzoni mwa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kukuingiza mabao mawili ya ushindi.

Bao la Liverpool lilifungwa na Daniel Sturridge (1-0) katika dakika ya 35. Bao la kusawazisha la Sevilla lilifungwa na Gameiro (1-1) katika dakika ya 45, Coke alihitimisha kwa bao la pili (1-2) katika dakika ya 64, kabla ya ya kufaulu kutumbukiza wavuni bao la tatu (1-3) katika dakika 70.

Wadadisi katika masuala ya soka wanabaini kwamba ushindi huu wa Sevilla utapelekea vilabu vya Uhispani kuongoza katika mashindano makubwa msimu huu.