KENYA-KPL-GOR MAHIA

KPL yaamuru Gor Mahia kupokonywa alama 3

Kamati ya nidhamu ya kampuni inayosimamia ligi kuu ya soka nchini Kenya KPL, imeamuru mabingwa watetezi wa ligi hiyo Gor Mahia ,kupokonywa alama tatu.

Wakati mchuano wa Mauritius dhidi ya Kenya katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018.
Wakati mchuano wa Mauritius dhidi ya Kenya katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018. AFP PHOTO / NICOLAS LARCHE
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya mashabiki wake kuzua fujo wake wa mchuano wake na Tusker FC mwezi Aprili katika uwanja wa Taifa wa Nyayo jijini Nairobi.

Mbali na adhabu hiyo kwa Gor Mahia, kipa wake Boniface Olouch amefungiwa kutocheza mchuano mmoja baada ya kumvamia mshika kibendera, mechi ambayo Tusker FC walishinda bao 1 kwa 0.

Kamati hiyo imebaini kuwa, klabu ya Gor Mahia ilishindwa kuwadhibiti mashabiki wake walioingia uwanjani na kuanza kumkimbiza mwamuzi msaidizi na kusimamisha mechi hiyo kwa dakika 10 baada ya Tusker kupewa penalti.

Pamoja na hilo, Kamati hiyo imesema haijaridhishwa na namna Gor Mahia inavyowadhibiti wachezaji wake wakati wa michuano mbalimbali na hivyo kuzua hofu uwanjani.