Bondia

Muhammad Ali afariki dunia

Nguli wa mchezo wa bondia Mohamed Ali siku za uhai wake.
Nguli wa mchezo wa bondia Mohamed Ali siku za uhai wake. Action Images / Sporting Pictures

Viongozi wa dunia na wapenzi wa mchezo wa bondia na wanamichezo wengine wameendelea kutoa risala za rambirambi na kumkumbuka nguli na aliyekuwa mwanabondia maarufu duniani Muhammad Ali ambaye amefariki dunia akiwa na miaka 74

Matangazo ya kibiashara

Kifo cha nguli huyo raia wa Marekani kilitangazwa na familia yake baada ya kulazwa hospitalini siku ya Alhamisi akisumbuliwa na tatizo la kupumua.

Ali pia amekuwa akisumbuliwa na maradhi aina ya Parkinson yanayomfanya mtu kutokuwa na uwezo wa kuwa mtulivu na mara nyingi kutetemeka.

Rais wa Marekani Barrack Obama amemwelezea Muhammmad Ali kama mwanabondia aliyeushangaza ulimwengu na kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri.

Naye rais wa zamani wa Marekani Billy Clinton amesema Ali, alikuwa mwanabondia aliyekuwa na ujasiri alipokuwa ulingoni na kuwatia moyo vijana wengi sana kuingia katika mchezo huu.

REUTERS/Kevin Lamarque

Pamoja na kwamba alikuwa mwanabondia, alikuwa pia mwanaharakati hasa kipindi cha kupambana na ubaguzi wa rangi nchini Marekani na anakumbukwa kupinga na kukataa kushiriki katika vita nchini Vietnam na kupokonywa mataji yake.

Atakumbukwa kuwa mwanabondia aliyefanya vizuri wakati wake katika karne ya Ishirini kati ya mwaka 1901 hadi 2000.

Mohamed Ali bat George Foreman à Kinshasa, le 30 octobre 1974. Il redevient ainsi champion du monde des poids lourds à 32 ans après que la justice l'a destitué de ses titres.
Mohamed Ali bat George Foreman à Kinshasa, le 30 octobre 1974. Il redevient ainsi champion du monde des poids lourds à 32 ans après que la justice l'a destitué de ses titres. AFP

Mambo muhimu kumhusu Muhammad Ali

 • Alizaliwa katika Familia ya Kikiristo na kupewa jina Marcellus Clay, lakini baadaye akabadilisha jina na kuwa Muislamu
 • Alizaliwa tarehe 17 mwezi Januari mwaka 1942.
 • Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74
 • Alishiriki katika mapigano 61 ya kulipwa kwa muda wa miaka 21
 • Alishinda mara 56 ikiwa ni pamoja na mapigano 37 kwa njia ya Knockout.
 • Alishinda mataji matatu katika uzani wa Heavyweight
 • Alishindwa mara 5.
 • Alishinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki katika uzani wa Light-Heavyweight mwaka 1960 mjini Rome nchini Italia.
 • Alipigana mapigano 31 akipata ushindi mfululizo na akashindwa kwa mara ya kwanza dhidi ya Joe Frazier mwaka 1971 katika pigano la Karne.
 • Mwaka 1974 alipata taji la dunia katika pambano maarufu la "Rumble in the Jungle" lililoandaliwa nchini Zaire jijini Kinshasa nchi ambayo siku hizi inaitwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kumshinda George Foreman.