TENESI

Djokovic awa mtu wanne kuweka historia ya kutwaa mataji makubwa

Novak Djokovic akiwa ameshika kikombe chake alichokabidhiwa baada ya kushinda taji la French Open 2016 dhidi ya Murray
Novak Djokovic akiwa ameshika kikombe chake alichokabidhiwa baada ya kushinda taji la French Open 2016 dhidi ya Murray RFI/Pierre René-Worms

Mchezaji nambari moja kwa mchezo wa tenesi duniani, Novak Djokovic ameshinda taji la French Open kwa mara ya 12, ambapo anakuwa mtu wa tatu kuweka historia ya kutwaa mataji manne makubwa "Grand Slams" kwa wakati mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Djokovic anaeshikilia nafasi ya kwanza kwenye mchezo wa tenesi kwa upande wa wanaume, amemfunga mpinzani wake wa siku nyingi, Andy Murray kwa seti 3-6, 6-1, 6-2 na 6-4 na kumuwezesha kushinda taji lake la 12 kubwa na kuungana na mchezaji, Don Budge aliyefanya hivyo mwaka 1938 na Rod Laver aliyefanya hivyo mwaka 1962 na 1969, wakiwa ni wachezaji pekee waliofanikiwa kushinda taji la French Open, Australian Open, US Open na Wimbledon mfululizo.

Djokovic mwenye umri wa miaka 29 hivi sasa, amejiweka kwenye nafasi nzuri ya kuweka rekodi ya kalenda ya michuano mikubwa "Grand Slams" iliyowahi kuwekwa na Laver miaka 47 iliyopita.

Andy Murray
Andy Murray RFI/Pierre René-Worms

Ushindi wa Djokovic hata hivyo haukuwa rahisi, baada ya kujikuta katika mchezo wa nane wa seti ya nne akipata wakati mgumu na kulazimika kutafuta alama 10 kabla ya kufanikiwa kupata ushindi kufuatia makosa aliyoyafanya Andy Murraye wakati akirejesha mpira akiupiga kwa nyuma.

Djokovic baada ya ushindi huo amesema "Ni wakati muhimu kwangu, na mkubwa katika historia yangu ya tenesi," alisema nguli huyu ambaye anakuwa mtu wa nane kufikia hatua ya kupata mataji mengi zaidi ya Grand Slams ambaye hata hivyo alishindwa kwenye fainali tatu zilizopita za French Open.

"Hivi leo nimejisikia kitu ambacho sijawahi kukisikia kwenye Roland Garros, nimeusikia upendo wa mashabiki," aliongeza Djokovic.

Novak Djokovic
Novak Djokovic RFI/Pierre René-Worms

Akihitimisha ushindi wake Djokovic alifanya ishara kma iliyowahi kufanywa na bingwa mara tatu wa michuano hii, Gustavo Kuerten kwa kuchora alama ya moyo mkubwa kwenye sakafu ya uwanja kabla ya kuanguka chini na kujilaza juu yake.

Akicheza kwenye fainali yake ya 20 ya mataji makubwa na mara ya sita mfululizo, mchezaji huyu mashuhuri raia wa Serbia, anakuwa mtu wa kwanza toka Jim Courier alivyofanya mwaka 1992 kushinda taji la Australian Open na French Open yakifuatana.

Ushindi huu pia unamuongezea ubavu dhidi ya mpinzani wake, kwa kuweka rekodi ya kumfunga mara nyingi zaidi katika fainali 8 kati ya mbili alizoshinda Murray.
Murray, mchezaji nambari mbili kwa ubora wa mchezo wa tenesi duniani, ni muingereza wa kwanza kufika hatua ya fainali ya French Open toka alipofanya hivyo muingereza mwenzake Bunny Austin mwaka 1937