EURO 2016-UFARANSA

Askari 180 wa kigeni kuimarisha ulinzi Euro 2016

Uwanja wa Matmut-Atlantique, unaotumiwa na klabu ya Girondins FC jijini Bordeaux.
Uwanja wa Matmut-Atlantique, unaotumiwa na klabu ya Girondins FC jijini Bordeaux. FRANCK FIFE / AFP

Askari polisi mia moja na themanini kutoka nchi zitakazoshiriki michuano ya Kombe la Ulaya (Euro-2016 ) wamewasili tangu Jumatatu nchini Ufaransa kusaidia kuwakamata wahuni, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa amesema.

Matangazo ya kibiashara

Bernard Cazeneuve amezindua kituo cha usirikiano wa polisi ya kimataifa (CCPI) katika mji wa Lognes (katika mkoa wa Paris), watakaohusika na "kutoa ulinzi" na kuzambaza habari katika muda wa shindano hilo."

Askari polisi 180 "kutoka" nchi 23 za kigeni zitakazoshiriki katika michuano ya Kombe la Ulaya (Euro,-2016) ikiwa ni pamoja na Ufaransa iliofuzu kama nchi itakayoandaa michuano hiyo, "waliwasili (Jumatatu) kuimarisha idadi" ya wenzao"wa Ufaransa Wazir Cazeneuve.

Askari hamsini watatumwa katika kituo hiki na watakua na wana "taarifa sahihi za vurugu zinazotokana na wafuasi kutoka nchi zao."Watasaidia kukomesha na kuzuia vurugu," kwa mujibu wa Bw Cazeneuve.

Wengine 130 watapelekwa katika miji kumi kwa "kusaidia" polisi ya Ufaransa, na kuunda timu za askari polisi ambao watakua imara kwa kupiga doria kila sehemu, huku wakipewa silaha na wakivalia sare, ili kubainika na kufuatilia wahuni wanaoweza kuibuka katika michuano hiyo.

"Serikali imechukua hatua kadhaa za kiutawala kupinga kuingia nchini Ufaransa kwa mashabiki wenye vurugu, ambao walipigwa marufuku kuingia katika viwanja nchini mwao, " Waziri Cazeneuve amesema kwa upande mwegine.

Vyanzo vya polisi vimebaini kwamba, mechi tano za Euro-2016 katika duru ya kwanza zitalindwa vilivyo. Mechi hizo ni pamoja na Uingereza - Urusi (Kundi B Juni 11 katika jiji la Marseille.), Uturuki - Croatia (Kundi D, Juni 12 katika jiji la Paris), Ujerumani - Poland (Kundi C, Juni 16 katika uwanja wa Stade de France), Uingereza- Wales (Kundi B, Juni 16 katika mji wa Lens) na Ukraine - Poland Kundi C Juni 21 katika jiji la Marseille).

Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuwa michuano hii ya Kombe la Ulaya (Euro-2016) itachezwa katika mazingira ya "kipekee kwa sababu tishio la kigaidi bado lipo katika kiwango cha juu sana. "