EURO 2016 - UHISPANIA

Del Bosque: Tupo kwenye kundi gumu lakini tutashinda

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa, Vicente del Bosque
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa, Vicente del Bosque REUTERS/Juan Medina

Timu ya taifa ya Uhispania inaendelea kujipanga kujaribu kutwaa taji la michuano ya Ulaya "Euro" lakini inakabiliwa na wakati mgumu kwenye kundi, ambapo kocha mkuu wa timu hiyo Vicente del Bosque amekiri timu yake kuwa kwenye mabadiliko. 

Matangazo ya kibiashara

Uhispania ambao ni mabingwa wa kombe la Ulaya mwaka 2008 na 2012, wanalenga kukwepa kutojirudia kwa kiwango kibaya walichoonesha wakati wa michuano ya kombe la dunia nchini Brazil miaka miwili iliyopita, ambapo kwenye kundi lake wako na timu za Croatia, Uturuki na Jamhuro ya Czech, kwenye kundi D.

Kocha wa Uhispania, Del Bosque amesema kuwa wanaenda kwenye michuano ya mwaka huu wakiwa na malengo makuu, nayo ni kuhakikisha wanatetea taji ambalo walilishinda miaka minne iliyopita.

Del Bosque ameongeza kuwa hali waliyonayo ni kama ile ya mwaka 2012 lakini sasa wanalenga zaidi kuwajibika uwanjani kwakuwa wanatetea mataji waliyoshinda mara mbili mfululiz, Bosque amesema haya wakati timu yake ikielekea kwenye mji wa Ile de Re uliko kwenye pwani ya Ufaransa.

Wachezaji wa timu ya taifa wakifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro
Wachezaji wa timu ya taifa wakifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro REUTERS/Javier Barbancho

"Lakini lazima tutofautishe kati ya malengo na kipi ni lazima. Kushinda taji la mwaka huu haiwezi kuwa ni jambo la lazima." alisema Del Bosque.

Del Bosque ameyasema haya huku akianisha kuwa timu yake inawakati mgumu kwakuwa iko kwenye mabadiliko toka ilipomaliza fainali za mwaka 2012.

Wachezaji 6 ambao walicheza kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Italia na timu hiyo kupata ushidi wa mabao 4-0, wanatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa awali wa timu hiyo dhidi ya Jamhuri ya Czech mjini Toulouse Jumatatu ya wiki ijayo.

Wachezaji hao wanaotarajiwa kupata nafasi ni pamoja na Koke, Alvaro Morata na Lucas Vazquez.

Lucas Vazquez anatajwa kama miongoni mwa wachezaji wenye kasi na wanaosumbua mabeki wa timu pinzani.

Uhispania itacheza mechi yake ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Croatia mjini Bordeaux.