EURO 2016

Chris Smalling awatoa hofu mashabiki wa Uingereza

Beki wa kati wa timu ya taifa ya Uingereza, Chris Smalling.
Beki wa kati wa timu ya taifa ya Uingereza, Chris Smalling. Reuters / Hannah McKay Livepic

Mlinzi wa kati wa timu ya taifa ya Uingereza, Chris Smalling, anatarajiwa kuanza tena mazoezi ya kawaida na wenzake hii leo licha ya kuondoka hapo jana kwenye uwanja wa mazoezi akiwa na jeraha la goti.

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo anayekipiga na klabu ya Manchester United, ni kiungo muhimu kwa kikosi cha kocha Roy Hodgson kinachoshiriki michuano ya mataifa Ulaya, alionesha ishara ya dole gumba kwa mashabiki wake kuashiria yuko vizuri.

Smalling ni miongoni mwa mabeki wa kati wanaopewa nafasi ya kucheza karibu mechi zote za hatua ya makundi ya kundi B na huenda akaanza dhidi ya Urusi Jumamosi ya wiki hii.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza, Daniel Sturridge.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza, Daniel Sturridge. Reuters / Lee Smith Livepic

Wakati huohuo mshambuliaji Daniel Sturridge ambaye amerejea hivi karibuni kwenye mazoezi ya kawaida na wenzake, amesema kuwa anamatarajio makubwa kwenye michuano ya mwaka huu na kwamba anauhakika wa kuisaidia timu yake.

Uingereza yenye wasatni wa wachezaji wenye umri wa miaka 25 na kuwa miongoni mwa vikosi vya timu zenye wachezaji vijana zaidi kwenye mashindani ya mwaka huu, Sturridge anasema umri haupaswi kuwa kigezo cha kuona kuwa hawatafanya vizuri kwenye michuano ya mwaka huu.

Mchezaji huyo ameongeza kuwa hawataogopa kucheza kwa kujituma na kwamba yaliyojiri kwenye michuano iliyopita hayatawakatisha tamaa kufanya vizuri mwaka huu.