NIGERIA-KESHI-SOKA

Stephen Keshi afariki dunia

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria, Stephen Keshi.
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria, Stephen Keshi. AFP PHOTO / PIUS UTOMI EKPEI

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria Stephen Keshi, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 54.

Matangazo ya kibiashara

Kifo cha Keshi ambaye aliingia katika vitabu vya historia kwa kuwa kocha na mchezaji wa zamani kuiongoza nchi yake kunyakua taji la ubingwa wa Afrika mwaka 2013, kilithibitishwa na Shirikisho la soka nchini humo NFF.

Vyombo vya Habari nchini Nigeria vinaripoti kuwa kifo cha Keshi kilishababishwa na mshtuko wa moyo.

Keshi pia aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Togo na Mali lakini aliwahi pia kucheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika klabu ya Anderlecht.

Mwaka 2014, aliingoza Nigeria hadi katika hatua ya 16 wakati wa michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.

Baada ya michuano ya kombe la dunia, alifutwa kazi lakini rais wa wakati huo Goodluck Jonathan aliamuru arejeshwe kazini.

Alifutwa kazi rasmi mwaka mwaka uliopita mwezi Julai.

Kifo cha kocha huyu kumeleta huzuni kubwa kwa wapenzi wa soka nchini Nigeria na barani Afrika.