EURO 2016

Wasifu wa timu zinazoshiriki fainali za Ulaya 2016, Ufaransa

DR

Kuanzia Juni 10 hadi Julai 11, nchi ya Ufaransa itakuwa mwenyeji wa fainali za kombe la Ulaya mwaka 2016, ambapo viwanja zaidi ya kumi kutumika kwenye fainali za mwaka huu, rfikiswahili itakuwa inakuletea kila kinachojiri kwenye michuano ya mwaka huu, na hapa unaweza kuzifahamu kwa undani timu zilizopata nafasi ya kushiriki fainali hizi.

Matangazo ya kibiashara

KUNDI A.

Albania Romania Ufaransa Uswizi
Timu ya taifa ya Ufaransa.

Ndio wenyeji wa michuano hii mwaka huu. Imekuwa ikishiriki katika michuano hii miaka yote isipokuwa mwaka 1988.Les Blues inatarajiwa kutumia uwanja wake wa nyumbani kushinda taji hili ambalo wameshinda mara mbili katika historia ya mashindano haya mwaka 1984 na 2000.

Kocha mkuu wa timu hii ni mfaransa, Didier Deschamps, wafungaji wa muda wote kwenye timu hii ni Thierry Henry aliyefunga mabao 51 na Karim Benzema aliyefunga mabao 27, rekodi ambayo anaishikilia hadi sasa.

Wachezaji waliowahi kuichezea timu hii kwa muda mrefu ni, Lilian Thuram aliyeichezea timu hiyo mara 142, Karim Benzema aliyeichezea timu yake mara 81 lakini hatashiriki katika michuano ya mwaka huu kutokana na kashfa ya mkanda wa ngono.

Mwaka 1984 iliponyakua taji hilo, Michel Platini rais wa zamani wa Uefa ndiye aliyekuwa tegemeo kwenye timu, ambapo wakati huo akiwa mchezaji aliifungia timu yake mabao 9.

Mwaka 2008 na 2010, Ufaransa ilifika katika hatua ya makundi lakini mwaka 2012 na 2014 ilifika katika hatua ya robo fainali, Ufaransa imecheza mechi 134 katika michuano ya Euro Imeshinda mechi 74, Imekwenda sare mara 34 na kupoteza mechi 26.

Timu ya taifa ya Albania.

Timu ya taifa ya Albania inashiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza, Kikosi hiki kinanolewa na kocha, Gianni De Biasi.

Wafungaji qa muda wote kwenye kikosi hiki cha Albania ni pamoja na, Erjon Bogdani ambaye ana mabao 18 na Hamdi Salihi mwenye mabao 11 rekodi ambayo anaishikilia hadi sasa.

Wachezaji waliocheza mechi nyingi zaidi wakiwa na timu ya taifa ya Albania ni pamoja na Lorik Cana aliyeichezea timu yake mara 87 na Lorik Canak amefunga mabao 87.

Timu hii ya Taifa imecheza mechi 93 za Kimataifa, Imeshinda mechi 18, Imetoka sare mara 22 na kupoteza mechi 53.

Timu ya taifa ya Romania.

Romania inarejea katika michuano hii baada ya kufika katika hatua ya robo fainali mwaka 2000 kwa kuifunga Uingereza mabao 3 kwa 2, kikosi hiki kinanolewa na kocha, Anghel Iordănescu.

Mfungaji bora katika historia ya soka nchini humo ni Gheorghe Hagi, Adrian Mutu ambao wamefunga mabao 35 lakini mfungaji anayeongoza kwa sasa ni Ciprian Marica mwenye mabao 25.

The Tricolours kama wanavyojulikana kwa jina lingine, ni mojawpao ya timu nne zilizoshiriki kwenye fainali ya kombe la dunia mara tatu kati ya mwaka 1930, 1934 na 1938.

Timu ya taifa Uswizi.

Nchi ambayo ndio makao makuu ya Shirikisho la soka duniani FIFA, mwaka 1996, 2004 na 2008 ilicheza katika michuano hii na kuondolewa katika hatua ya makundi.

Kocha wa timu hii ni, Vladimir Petkovic.

Wafungaji bora katika historia ya soka nchini humo ni, Alexander Frei mwenye mabao 42 lakini mfungaji bora wa sasa ni Xherdan Shaqiri ambaye amefunga mabao 17.

Mchezaji aliyewahi kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu ni Heinz Hermann mara 118, lakini anayeongoza kwa sasa ni Gokhan Inler ambaye amecheza mara 89.

Uswizi imecheza mechi 101 za Kimataifa. Imeshinda mechi 40 na kutoka sare mara 24, mwaka 2012, ilishindwa kufuzu baada ya kushindwa mikononi mwa Uingereza na Montenegro.

 

KUNDI B
Uingereza Urusi Wales Slovakia

Timu ya taifa Uingereza.

Haijawahi kushinda taji la bara Ulaya licha ya kushinda kombe la dunia mara moja mwaka 1966, mara ya mwisho kufanya vizuri ilikuwa ni mwaka 1968 na 1996 ilipofika katika hatua ya nusu fainali ya michuano hii.

Kocha wa timi hii ni Roy Hodgson.

Wafungaji bora miaka ya zamani na hivi sasa ni Wayne Rooney ambaye amefunga mabao 51, pamoja na Sir Bob Charlton aliyefunga mabao 50.

Mchezaji aliyeichezea timu hii kwa muda mrefu ni Peter Shilton ambaye amecheza mara 125 na miaka ya hivi karibuni ni Wayne Rooney ambaye amecheza mara 109.

Timu hii inayofahamika pia kwa jina la Three Lions ilifuzu katika michuano hii ya bara Ulaya kwa kushinda mechi zake zote 10 za kufuzu.

Katika michuano 127 ya Kimataifa iliyocheza, imeshinda mara 75, kwenda sare mara 33 na kupoteza mechi 19.

Timu ya taifa Urusi.

Urusi imekuwa ikifuzu mara kwa mara katika michuano hii na ilishinda fainali hizi mwaka 1960, na ikamaliza kwenye nafasi ya pili mwaka 1964, 1972 na 1988m kikosi hiki kinanolewa na Leonid Slutski.

Mfugaji bora wakati wote kwenye timu hii ni Oleh Blokhin ambaye aliwahi kufunga mabao 42 lakini mchezaji wa sasa anayeongoza ni Aleksandr Kerzhakov ambaye ana mabao 30.

Mchezaji aliyewahi kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu ni Sergei Ignashevich ambaye amecheza mechi 114 hadi sasa.

Timu ya taifa ya Urusi imecheza mechi 150, imeshinda mara 85, imeshindwa mara 35 na kupoteza mechi 30.

Timu ya taifa Slovakia.

Ilishinda taji hili mwaka 1976 baada ya kuishinda Ujerumani Magharibi wakati huo ikiitwa Czechoslovakia, hii ni mara kwanza kwa Slovakia kushiriki fainali za Ulaya ikiwa ni taifa huru.

Kocha wa timu hii ni Jan Kozak.

Mfungaji bora wa muda wote kwenye timu hii ni Robert Vittek ambaye hadi sasa amefunga mabao 23, mchezaji ambaye ameichezea nchi hii kwa muda mrefu zaidi ni Miroslav Karhan ambaye amecheza mara 107 na miaka ya hivi karibuni ni Marek Hamsik mara 83.

Inasaka taji lake la kwanza katika michuano hii.

Kwa ujumla imecheza mechi 124, imeshinda 62, imetoka sare mara 26 na kupoteza mechi 36.

Timu ya taifa Wales.

Hii ndio mara ya kwanza inashiriki katika mashindano makubwa kama haya kwa kipindi cha nusu karne.

Mshambuliaji Gareth Bale anasalia mchezaji muhimu aliyeisaidia nchi hii kufuzu katika fainali hii.

Kocha wa timu hii ni: Chris Coleman.

Mfungaji bora katika historia ya timu hiyo ni Ian Rush ambaye ana mabao 28 lakini anayeongoza kwa sasa katika ufungaji wa mabao ni Gareth Bale ambaye ana mabao 19.

Mchezaji ambaye ameichezea timu hii kwa muda mrefu inayofahamika kwa jina maarufu la Dragons, ni Neville Southall amecheza mara 92 lakini mchezaji anayeongoza kwa sasa ni Chris Gunter ambaye amcheza mara 64.

Mara ya mwisho kushiriki katika mashindano makubwa ilikuwa ni wakati wa kombe la dunia mwaka 1958.

 

KUNDI C

Ujerumani Ireland Kaskazini Ukraine Poland

Timu ya taifa Ujerumani.

Ni bingwa wa soka barani Ulaya, haikufuzu katika fainali hizi mara moja katika historia yake ya soka, ilishinda taji hili mwaka 1972 na 1980 wakati huo ikifahamika kuwa Ujerumani Magharibi lakini pia ilishinda mwaka 1996.

Kocha wa timu hii ni Joachim Low.

Mfungaji bora anayeshikilia historia ni Miroslav Klose ambaye ana mabao 71 lakini mfungaji bora wa sasa ni Lukas Podolski ambaye ana mabao 48.
 

Lothar Mathaus anasalia kuwa mchezaji aliyewahi kuichezea Ujerumani kwa muda mrefu mara 150 huku Lukas Podolski akiwa wa pili kwa sasa na kuweka rekodi ya mechi 126.

Katika mechi 141 ilizocheza, imeshinda mechi 92 na imekwenda sare mara 30 na kufungwa mara 19.

Timu ya taifa Ireland Kaskazini.

Inashiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza, ilimaliza katika nafasi ya kwanza katika michuano ya kufuzu kucheza fainali hii ya bara Ulaya.

Kocha wa timi huu ni Michael O'Neill.

Mfungaji bora kihistoria ni David Healy ambaye aliifunga mabao 36, lakini mfungaji bora wa sasa ni Kyle Lafferty ambaye ametikisa nyavu mara 16.

Pat Jennings ndiye mchezaji aliyeichezea nchi hiyo kwa muda mrefu wa mechi 119 lakini Aaron Hughes anaongoza kwa sasa akiwa amecheza mechi 96.

Katika mechi 110 ilizocheza, imeshinda 40 imetika sare mara 25 na imepoteza mara 45.

Timu ya taifa Poland.

Inashiriki kwa mara ya kwanza katika michuano hii tangu kushiriki mara ya kwanza mwaka 2008, mwaka 2012 ilishirikiana na Ukraine kuandaa michuano hii na kumaliza wa mwisho katika kundi lake.

Kocha ni Adam Nawalka.

Mfungaji bora anayeshikilia historia ni Włodzimierz Lubański ambaye ana mabao 48 lakini Robert Lewandowski anaongoza kikosi cha sasa kwa mabao 34.
Michal Zewlakow anasalia mchezaji aliweka historia kwa kuichezea nchi yake mara 102 lakini mchezaji wa sasa ni akub Błaszczykowski ambaye ameichezea nchi yake mara 75.
Katika mechi 106 ilizocheza hadi sasa, imeshinda mechi 44, imekwenda sare mara 30 na kupoteza mechi 32.

Timu ya taifa Ukraine.

Ilishiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza mwaka 2012 iliposhrikiana na Poland kuwa wenyeji, mwaka 2012 ilifika katika hatua ya makundi.

Kocha wa kikosi hiki ni Mykhailo Fomenko.

Mfungaji bora anayeshikilia historia ni Andriy Shevchenko ambaye alitkisa nyavu mara 48, lakini mchezaji anayeongoza kwa sasa ni Andriy Yarmolenko amabye ana mabao 22.

Anatoliy Tymoshchuk anasalia kuwa mchezaji anayeshikilia rekodi ya kuichezea nchi yake mara 141 na hakuna aliyefikia rekodi hiyo hadi sasa.

Baadhi ya matokeo ya michuano ya kufuzu kucheza fainali hii, 14/11/2015: Ukraine 2 Slovenia 0, 11/06/2012: Ukraine 2 Sweden 1, 09/10/1999: Russia 1-1 Ukraine, fainali ya UEFA EURO mwaka 2000

 

KUNDI D.
Croatia Jamhuri ya Czech Uhispania Uturuki

Timu ya taifa Croatia.

Matokeo mazuri iliyowahi kuyapata ni kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro, mwaka 1996 na 2008.

Kikosi cha Croatia kinaongozwa na kocha, Ante Cecic, na mfungaji mabao wa muda wote wa timu ya taifa ya Croatia ni Davor Suker aliyefunga mabao 45, na kwasasa mfungaji bora ni Darijo Srna mwenye bao 21.

Mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi akiwa na timu hii ya taifa ni Darijo Srna aliyeichezea mara 127 mpaka sasa. Jina la utani la timu hii ni Kockasti na uwanja wake wa nyumbani ni Maksimir ulioko mjini Zagreb.

Toka kujitenga kutoka kwa iliyokuwa Yugoslavia mwaka 1991, Croatia imekuwa miongoni mwa timu bora zaidi kwenye soka la kimataifa, ambapo walifuzu kwa mara yao ya kwanza kabisa kwenye kombe la Ulaya na harakati za kombe la dunia na kisha kumaliza kwenye nafasi ya tatu wakati wa fainali za kombe la dunia nchini Ufaransa mwaka 1998 ambapo Davor Suker aliibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 6.

Croatia imekuwa mshiriki wa mara kwa mara kwenye michuano hii mikubwa duniani ambapo ilikosa mwaka 2000 na 2010 pekee lakini wamefanikiwa kufuzu hatua za juu kwenye michuano ya Euro mwaka 2008 na kufuzu kwenye fainali za mwaka 2016, ikiwa ni mara yao ya nne mfululizo na wakimaliza kwenye nafasi ya pili kwenye hatua ya makundi kufuzu nyuma ya Italia.

Timu hii ya taifa kiujumla imecheza mechi 76, imeshinda 46, imetoka sare mara 18, imepoteza mara 12, imefunga mabao 136 na kufungwa mabao 55.
 

Timu ya taifa Jamhuri ya Czech.

Matokoe mazuri ambayo timu ya taifa ya Czech imewahi kuyapata ni wakati iliposhiriki michuano ya kombe la Ulaya mwaka 1976 na kuwa mabingwa, wakati huo ilikuwa ikifahamika kama Czechoslovakia.

Kikosi cha timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech kinanolewa na kocha Pavel Vrba.

Mchezaji anayeongoza kwa ufungaji mabao akiwa na timu yake ya taifa kwenye kikosi hiki ni mkongwe Jan Koller, ambaye amestaafu soka akiwa ameshaifungia timu yake ya taifa mabao 55, na kwa sasa mfungaji anayoengoza kwa mabao kwenye timu hii ni Tomas Rosicky mwenye mabao 22.

Wachezaji wa timu hii ambao wamecheza mechi nyingi zaidi ni pamoja na Karel Poborsky na Peter Cech waliocheza mechi 118, huku kwa sasa rekodi hiyo ikishikiliwa na mlinda mlango anayechezea klabu ya Arsenal ya Uingereza, Peter Cech aliyecheza mechi 118 akiwa na timu ya taifa.

Shirikisho la soka la Jamhuri ya Czech liliundwa mwaka 1901. Timu hii inafahamika kwa jina jingine kama Narodni Tym ikimaanisha timu ya taifa, imekuwa ikicheza mechi zake za kimataifa kwenye viwanja tofautitofauti.

Timu hii ya taifa imeanza kushiriki kwenye kombe la Ulaya kama taifa huru mwaka 1994 na toka wakati huo, timu hii imekuwa ikifuzu kushiriki michuanp yote inayoandaliwa na shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA, ambapo ilimaliza kwenye nafasi ya pili kwenye michuano ya mwaka 1996 yakiwa ni mashindano yake ya kwanza makubwa kushiriki, na pia kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mwaka 2004.

Hata hivyo matokeo ya mechi za kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia kwa timu hii sio mazuri sana, ambapo kwenye fainali za mwaka 2006 zilizofanyika nchini Ujerumani, waliondolewa kwenye hatua ya makundi.

Timu hii wakati ikitwaa taji la Ulaya mwaka 1976, iliifunga timu ya taifa ya Ujerumani Magharibi kwa njia ya matuta na kwa mara mbili mfululizo walifungwa kwenye hatua ya fainali wakatik wa kombe la dunia la mwaka 1934 na 1962, wakati huo ikishiriki kama Czechoslovakia.

Kiujumla timu hii imecheza mechi takribani 145, imeshinda mechi 89, ikatoa sare 26, ikapoteza mechi 30, imefunga mabao 278 na kukubali nyavu zake kutikiswa mara 129.

Jamhuri ya Czech ilifika hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Euro ya mwaka 2012, ikiwa ni mara yake ya tano kushiriki fainali hizo toka mwaka 1993 ilipojitenga kutoka Czechoslovakia. Ilipoteza kwenye mchezo wake wa fainali za Euro mwaka 1996 dhidi ya Ujerumani, ambapo bao la mkongwe Oliver Bierhoffs lilitosha kufanikisha ushindi wa Ujerumani wa mabao 2-1, ambapo ilipata matokeo kama hayo miaka nane baadae ilipocheza na Ugiriki kwenye hatua ya nne.

Timu ya taifa Uhispania.

Matokeo mazuri ambayo timu hii iliwahi kuyaandikisha ni kwenye fainali za mwaka 1964, 2008 na 2012. Kikosi hiki kinanolewa na kocha Vicente de Bosque.

Mchezaji pekee anayeongoza kwa kupachika mabao akiwa na kikosi hiki ni mshambuliaji anayekipiga kwenye klabu ya Manchester City, David Silva ambaye amepachika mabao 59, na sasa anaongoza pia kwa kupachika mabao mengi ambapo ana mabao 23.

Mchezaji pekee anayeongoza kwa kucheza mechi nyingi zaidi akiwa na timu yake ya taifa ni mlinda mlango wa zamani wa Real Madrid ya Uhispania, Iker Casillas, ambaye amecheza mechi 1656 rekodi ambayo anaishikilia hadi sasa.

Timu ya taifa ya Uhispania inafahamika kama La Roja ama “Wekundu”, na imekuwa ikitumia viwanja mbalimbali kucheza mechi zake za kimataifa. Shirikisho lake la mpira lilianzishwa mwaka 1909.

Baada ya miongo kadhaa ya kutofanya vizuri kwenye michuano hii ya Ulaya lakini ikafanikiwa kulitwaa taji hilo kwenye fainali za mwaka 1964 zilizofanyika kwenye ardhi yake ya nyumbani, timu ya taifa ya Uhispania mara moja ikaanza kutawala soka la dunia.

Kwenye fainali za Ulaya za mwaka 2008 ambazo walifanikiwa kushinda taji hilo baada ya kuifunga timu ya taifa ya Ujerumani kwa bao 1-0, ilifuatiwa na ushindi wa kombe la dunia miaka miwili baadae kwenye fainali zilizofanyika Afrika Kusini, kikosi hiki cha Vicente del Bosque kikiwa ni timu ya kwanza kufanikiwa kutwaa taji la kombe la dunia kwa nchi kutoka Ulaya kuchukua taji hilo nje ya ardhi yake.

Historia zaidi waliiweka kwenye mwaka 2012 walipotwaa taji la Ulaya na kuwa timu ya kwanza kufanikiwa kutetea taji hilo kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Italia, licha ya mbio zao za kutaka kutetea kombe la dunia zilikatizwa kwenye hatua ya makundi miaka miwili baadae.

Kiujumla timu hii imecheza mechi takribani 151, ikipata ushindi kwenye mechi 98, ikitoa sare mechi 27, ikipoteza michezo 26, ikifunga mabao 333 na kufungwa mabao 118.

Uhaba wa mataji kwa timu hii ulimalizwa mwaka 2008 mjini Vienna ambapo kikosi cha Luis Aragones kilipata ushindi dhidi ya Ujerumani, huku mshambuliaji wake Fernando Torres akiwa muuaji wa mabao kwenye kwenye mechi zote ambapo miaka minne baadae akawa mchezaji pekee aliyefunga kwenye fainali za Euro akiwa na Uhispania ambayo sasa inanolewa na Vicent del Bosque.

Timu ya taifa Uturuki.

Matokeo mazuri ambayo timu hii imewahi kuyapata ni katika fainali za mwaka 2008. Kikosi hiki kinanolewa na kocha Fatih Terim.

Wachezaji wanaoongoza kwa ufungaji wa mabao wakiwa na timu yao ya taifa ni, Hakan Sukur aliyefunga mabao 51 na sasa mchezaji anayeoongoza wa ufungaji wa mabao ni, Burak Yilmaz mwenye mabao 19.

Wachezaji waliocheza mechi nyingi zaidi kwenye kikosi hiki ni pamoja na Rustu Recber aliyecheza mechi 120 na kwasasa mchezaji anayeshikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi ni, Emre Belozoglu aliyecheza mechi 93.

Timu hii inafahamika kwa jina la utani kama Ay Yildizhlar ama msalaba wa nyota, mechi zake imekuwa ikitumia viwanja mbalmbali.

Mafanikio makubwa ya Uturuki iliyapata kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 2002, ambapo kikosi kilichokuwa kinanolewa na Senol Gunes kilifanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya tatu. Na fainali hizi zilikuwa ni fainali zake za pili kushiriki na toka wakati huo haijawahi kushiriki fainal nyingine zilizofuata.

Ilichukua majaribio zaidi ya 10 kwa timu ya taifa ya Uturuki kufanikiwa kufuzu kwenye fainali zake za kwanza za michuano ya Ulaya, na baada ya kupoteza mechi zake zote tatu mfululizo kwenye fainali za mwaka 1996, walifika kwenye hatua ya robo fainali za kombe la Ulaya la mwaka 2000 wakati kikinolewa na kocha Mustafa Denizli.

Timu hii ilipiga hatua zaidi miaka nane baadae nchini Austria na Uswis ambapo kwenye hatua ya matuta walifanikiwa kupata ushindi dhidi ya Croatia na kutinga hatua ya nusu fainali, ambapo walipoteza mchezo wao dhidi ya Ujerumani kwa kufungwa mabao 3-2. Baada ya kukosa kushiriki fainali zilizoandaliwa kwa pamoja na nchi za Polans na Ukraine, wamerejea kwenye fainali za mwaka huu zinazofanyika nchini Ufaransa.

Kiujumla timu hii imecheza mechi 122, imepata ushindi kwenye mechi 47, imepata sare mechi 29, imepoteza mechi 46, imefunga mabao 145 na nyavu zake kutikiswa mara 167. Baada ya kushindwa kufuzu kwenye awamu mbili ilizojaribu, walirejea kwenye fainali za mwaka 1996 lakini wakashindwa kupata alama yoyote kwenye fainali hizo zilizofanyika Uingereza. Walifuzu fainali za mwaka 2000 na kufuzu hatua ya makundi kabla ya kuondolewa kwenye hatua ya robo fainali na Ureno.

Mwaka 2004 timu hii ilishindwa kufuzu lakini ikafanikiwa kurejea kwenye fainali za mwaka 2008 ambapo walifika hatua ya nusu fainali na kukutana na Ujerumani. Licha ya kufanya vizuri kwenye mechi za kufuzu fainali za mwaka 2012 timu hiyo ilifungwa na Ujermani lakini ikamaliza kwenye nafasi ya pili kwenye hatua ya makundi.

 

KUNDI E
Ubelgiji Italia Jamhuri ya Ireland Sweden

Timu ya taifa Ubelgiji.

Matokeo bora zaidi ambayo timu hii ya taifa imewahi kuyaandikisha ni mwaka 1980. Kikosi cha Ubelgiji kwa sasa kinanolewa na kocha Marc Wilmots.

Wachezaji wanaoshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi wakiwa na timu hii ya taifa ni pamoja na Bernard Voorhoof na Paul Van Himst walofunga mabao 30 kila mmoja huku kwa sasa mchezaji anayeoongoza ni Marouane Fellaini mwenye mabao 15.

Wachezaji wa muda wote waliocheza mechi nyingi zaidi na kikosi hiki ni pamoja na Jan Ceulemans aliyecheza mechi 96 na sasa mchezaji Jan Vertonghen anaongoza akiwa amecheza mechi 76. Timu hii inafahamika kwa jina la utani kama Rode Duivels au Diales Rouge ikiwa na maana ya “Mashetani wekundu”.

Inatumia uwanja wa Roi Baudouin ulioko jijini Brussels kucheza mechi zake za kimataifa.

Timu ya taifa ya Ubelgiji ilimaliza ukame wake wa miaka 12 wa kutoshiriki mashindani makubwa, kwa kufanya vizuri kwneye mechi za kufuzu na kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 nchini Brazil na kufika kwenye hatua ya 8 bora.

Mafanikio ya kombe la dunia la mwaka 2014 yameisaidia pia timu hiyo kufanya vizuri zaidi kwenye mechi za kufuzu kucheza fainali za Ulaya mwaka huu kwakumaliza kwenye nafasi ya kwanza kwenye kundi lake.

Kwenye fainali za mwaka huu wanatarajia kufanya vizuri kidogo ama zaidi kama walivyowahi kufanya vizuri kwenye fainali za kombe la Ulaya mwaka 1980 na kumaliza kwenye nafasi ya nne katika fainali za kombe la dunia mwaka 1986.

Kiujumla timu hii imecheza mechi 116, imefanikiwa kupata ushindi kwenye mechi 53, ikatoka sare mara 28, ikapoteza mechi 35, imefunga mabao 183 na kufungwa mabao 132. Ubelgiji sasa imekuwa timu tishio kwenye ukanda wa Ulaya na kumaliza ukame wa miongo mitatu, ambapo walikuwa hawajawahi kukosa kushiriki kwenye miaka ya 1970 na 1980.

Walimaliza kwenye nafasi ya tatu katika fainali za Ulaya zilizofanyika kwenye ardhi yake mwaka 1972 na miaka 8 baadae almanusura watwae taji hilo lakini wakapoteza mbele ya Ujerumani.

Timu ya taifa Italia.

Matokeo mazuri zaidi ambayo timu hii ya taifa imewahi kuyaandikisha ni kwenye fainali za mwaka 1968 za kombe la Ulaya. Kikosi hiki kinanolewa na kocha Antonio Conte.

Wafungaji wa muda wotwe kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Italia ni pamoja na Luigi Riva aliyefunga mabao 35, ambapo sasa rekodi hiyo inashikiliwa na Daniel De Rossi aliyefunga mabao 17.

Mchezaji waliyeweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi akiwa na timu yake ya taifa ni mlinda mlango wa timu hiyo na klabu ya Juventus ya Italia, Gianluig Buffon aliyecheza mechi 154 akiwa na timu yake ya taifa, rekodi ambayo bado anaishikilia hadi sasa. Jina la utani la timu hii ni Azzurri ikiwanna maana ya Kijani.

Timu inatumia viwanja mbalimbali inapocheza mechi zake za kimataifa. Timu ya taifa ya Italia ambayo inatajwa kuwa miongoni mwa timu bora zaidi kuwahi kucheza kwenye fainali za kombe la dunia na kulitwaa mara nne kwenye fainali za mwaka 1934, 1938, 1982 na 2006, timu hii imekuwa mabingwa wa kombe la Ulaya mara moja pekee wakati iliposhiriki mwaka 1968.

Toka wakati huo haijawahi na wakati mzuri kwenye fainali za Ulaya, kwa kushindwa kufuzu fainali za mwaka 1984 na zile za 1992 lakini ikafika hatua ya fainali kwenye fainali za mwaka 2000 na 2012. Timu hii imefuzu kwenye michuano ya mwaka huu bila ya kupoteza mchezo wowote kwenye hatua ya makundi.

Kiujumla timu hii imecheza mechi 141, ikafanikiwa kupata ushindi kwenye mechi 77, ikitoka sare mechi 45, ikipoteza mechi 19, ikifanikiwa kufunga mabao 220 na kufungwa mabao 97.

Mafanikio pekee ya timu hii kwenye fainali za Ulaya yalipatikana mwaka 1968 ikiwa chini ya kocha Ferriccio Valcareggi, ambapo waliifunga Yugoslavia kwa mabao 2-0.

Timu hii ilijaribu kutwa taji hili kwenye fainalu za mwaka 2000 ambapo walipoteza mchezo wao wa fainali mbele ya Ufaransa, ambapo mshambuliaji David Trezeguet alikuwa muuaji wao bao la muda wa nyongeza.

Timu hii haikufanya vizuri kwenye fainali za mwaka 2012 ambapo walipoteza dhidi ya Uhispania kwa mabao 4-0, walifanikiwa kufika hatua ya nusu fainali za mwaka 1980 na 1988 ambapo Italia imefanikiwa kufika kila fainali za kombe la Ulaya toka mwaka 1992

Timu ya taifa Jamhuri ya Ireland.

Matokeo mazuri zaidi ambayo timu hii ya taifa ya Jamhuri ya Ireland imewahi kuyaandikisha ni wakati iliposhiriki fainali za mwaka 1988 na zile za mwaka 2012. Kikosi hiki sasa kinanolewa na kocha Martin O'Neill.

Mchezaji pekee anayeongoza kufunga mabao mwengi zaidi akiwa na timu yake ya taifa ni Robbie Keane aliyefunga mabao 67, rekodi ambayo bado anaishikilia hadi sasa. Robbie Keane pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyecheza mechi nyingi zaidi kwenye timu yake ya taifa, akiwa amecheza mechi 143.

Timu ya Jamhuri ya Ireland inafahamika kwa jina la utani kama Boys in Green, na imekuwa ikicheza mechi zake za kimataifa kwenye uwanja wa Dublin Arena.

Jamhuri ya Ireland ilianza kuonekana kwenye mashindano ya kimataifa mwaka 1988 na kukumbukwa kwa kuifunga Uingereza na kushindwa kufurukuta mbele ya mabingwa Uholanzi kwenye hatua ya nne bora.

Kocha muingereza Jack Charlton alifanikiwa kuipeleka timu hiyi kushiriki kwenye fainali zilizofuata za kombe la dunia, ikiwa ni kombe la kwanza kushiriki nchini Italia na kufika hatua ya robo fainali.

Ilifanikiwa kucheza fainali yake ya tatu ya kombe la dunia mwaka 2002 lakini ikashindwa kurejea kucheza fainali za Ulaya za mwaka 2012, ambapo kikosi hiki cha Giovanni Trapattoni kilipoteza mechi zake zote tatu za hatua ya makundi.

Kiujumla timu hii imecheza mechi 127, ikapata ushindi mara 51, ikatoa sare mara 37, ikapoteza mechi 39, imefunga mabao 186 na kufungwa mabao 147.

Mara yake ya kwanza kushiriki kwenye fainali za kombe la Ulaya ni mwaka 1988 na kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Uingereza.

Jamhuri ya Ireland ilishindwa kufuzu kucheza fainali za mwaka 1992 na kupoteza kwenye mechi za kufuzu dhidi ya Uholanzi an Uturuki mwaka 1996 na 2000, walimaliza kwenye nafasi ya tatu kwenye mechi zake za kufuzu za mwaka 2004 na 2008 lakini ikafika fainali za mwaka 2012.

Timu ya taifa Sweden.

Matokeo mazuri zaidi ambayo timu hii imewahi kuyaandikisha ni mwaka 1992 ilipocheza fainali za kombe la Ulaya, Kikosi hiki sasa kinanolewa na kocha Erik Hamren.

Mfungaji wa muda wote anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi akiwa na timu ya taifa ni Zlatan Ibrahimovic ambaye amefunga mabao 62. Mchezaji anayeongoza kwa kucheza mechi nyingi zaidi kwenye timu ya taifa ya Sweden ni Anders Svensson aliyecheza mechi 148 rekodi ambayo anaishikilia hadi sasa.

Timu ya taifa ya Swedn inafahamika kwa jina la utani kama Blagult ikiwa na maana ya Kijani na Njano, uwanja ambao unatumiwa kwa mechi za kimataifa na timu hii ni uwanja wa Friends Arena ulioko Solna.

Sweden ndio taifa pekee ambalo liliandaa fainali za kombe la dunia kwenye ardhi yake na kupoteza kwenye mchezo wa fainali, timu hii haijawahi kufikia rekodi iliyowahi kuiweka mwaka 1958, lakini ikafanikiwa kushiriki kwenye michuano minne iliyoshiriki, huku fainali za Ulaya za mwaka 1992 zikiwa ni fainali zake za kwanza za mabara, walishika nafasi ya tatu kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 1994 licha ya kushindwa kufuzu kwenye fainali mbili zilizopita.

Timu hii imefanikiw akucheza kwenye fainali tano za kombe la Ulaya.

Timu hii imecheza mechi 121 na kushinda mechi 59, ikitoka sare mechi 29, na kupoteza mechi 32, huku ikifanikiwa kufunga mabao 198 na kukubali nyavu zake kutikiswa mara 126.

Sweden ilifika hatua ya nusu fainali za mashindano ya mwaka 1992 wakati michuano hiyo ilipoandaliwa kwenye ardhi yake.

Mwaka 2000 ilifanikiwa kufuzu kwenye fainali za Ulaya lakini toka wakati huo haijawahi kushiriki. Mwaka 2004 iliondolewa kwenye fainali za Ulaya hata bila ya kupoteza mechi yoyote.

 

KUNDI F
Austria Hungary Iceland Portugal

Timu ya taifa ya Australia.

Matokeo mazuri zaidi ambayo timu hii imewahi kurekodi ni yale ya kwenye fainali za kombe la Ulaya mwaka 2008. Kikosi hiki sasa kinanolewa na kocha Marcel Koller.

Wafungaji wa muda wote wakiwa na timu ya taifa ya Australia ni pamoja na Toni Polster aliyefunga mabao 44 na kwasasa rekodi ya ufungaji bora inashikiliwa na mchezaji Marc Janko mwenye mabao 25.

Wachezaji waliocheza mechi nyingi zaidi wakiwa na timu ya taifa ya Australia ni pamoja na Andreas Herzog aliyecheza mechi 103 na sasa mchezaji Christian Fuchs anashikilia rekodi hiyo kwa kucheza mechi 72.

Timu hii haina jina lolote la utani, Uwanja ambao imekuwa ikiutumia kwa mechi zake za kimataifa ni uwanja wa Ernst-Happel-Stadion ulioko mjini Vienna. Historia ya timu hii kwenye mashindano ya kimataifa ni ya muda mrefu, ambapo ilimaliza kwenye nafasi ya tatu kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 1954 na baada ya hapo imeshashiriki fainali 7 za kombe la dunia na mara ya mwisho ilikuwa ni kwenye fainali za mwaka 1998.

Timu hii imecheza mechi 103 na kufanikiwa kupata ushindi mara 45, kutoka sare mara 18 na kupoteza mechi 40 na kufunga mabao 185 na kufungwa mabao 150. Fainali za mwaka 2008 na baada ya kunyakua kombe, zimebaki kuwa fainali pekee kwa nchi kupata mafanikio kwenye jukwaa la kimataifa.

Fainali za mwaka huu ni muhimu kwa timu hii kwakuwa haijawahi kufuzu kwenye fainali nying toka iliposhiriki fainali za mwaka 2012.

Timu ya taifa Hungary.

Matokeo mazuri ambayo timu hii imeshawahi kuyarekodi ni yale ya kwenye fainali za Ulaya za mwaka 1964. Kikosi hiki kinanolewa na kocha Bernd Storck.

Wafungaji wa muda wote kwenye timu ya taifa ya Hungary ni pamoja na Ferenc Pukas aliyefunga mabao 84 na sasa rekodi hiyo inashikiliwa na Zoltan Gera mwenye mabao 24.

Wachezaji waliocheza mechi nyingi zaidi wakiwa na timu ya taifa ni pamoja na Jozsef Bozsiki aliyefunga mabao 101 na sasa rekodi hiyo inashikiliwa na Gabor Kiraly mwenye mabao 100.

Jina la utani la timu hii ni Mighty Magyars. Uwanja wa nyumbani ambao imekuwa ikiutumi kwenye mechi zake za kimataifa ni Groupama Arena ulioko Budapest.

Timu hii ambayo wakati fulani ilikuwa vinara kwenye soka la Ulaya na la dunia, ilimaliza kwenye nafasi ya pili kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 1938 na 1954 na kufanikiwa kutwaa mataji matatu ya Olympic, nchi hii imeshindwa kufuzu kwenye mashindan0 14 makubwa baada ya kucheza fainali za mwaka 1986 na kufuzu kwa bahati kwenye fainali za mwaka huu za kombe la Ulaya.

Kizazi cha dhahabu cha wachezaji kama Ferenc Puskas, Jozsef Bozsik, Sandor Kocsic na kikosi chote kilichokuwa kinaongozwa na Mighty Magayars na kufanya makubwa kwenye miaka ya 1950, yote haya yamebaki kuwa historia.

Kiujumla timu hii imecheza mechi 125, imepata ushindi kwenye mechi 53 ilizocheza, imetoka sare mara 26, imepoteza mechi 46, imefunga mabao 202 na kufungwa mabao 167. Mchezaji Florian Albert aliisaidia timu yake kumaliza kwenye nafasi ya tatu kwenye fainali za mwaka 1964 na nafasi ya nne kwenye fainali za mwaka 1972.

Mwaka 1964 walifanikiwa kuwafunga Wales, Ujerumani mashariki na Ufaransa kabla ya kufungwa mabao 2-1 kwenye muda wa nyongeza na timu ya taifa ya Uhispania.
Majaribio 10 yaliyopita ya timu ya taifa ya Hungary kujaribu kufuzu kucheza fainali za kombe la Ulaya yamefanyika bila mafanikio, licha ya kumaliza kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Uholanzi na Sweden kwenye fainali za Ulaya za mwaka 2012.

 
Timu ya taifa Iceland.

Timu hii haijawahi kufuzu kucheza fainali hizi hapo kabla. Kikosi hiki kinafundishwa na Lars Lagerback na Heimir Hallgrimsson.

Mfungaji wa muda wote anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi akiwa na timu ya taifa ya Iceland ni Eidur Gudjohsen mwenye mabao 25, rekodi ambayo anaishikilia hadi leo.

Wachezaji waliocheza mechi nyingi zaidi wakiwa na timu ya taifa ya Iceland ni pamoja na Runar Kristinsson aliyecheza mechi 104 pamoja na Eidur Gudjohnsen aliyecheza mechi 81.

Timu ya taifa ya Iceland inafahamika kwa jina la utani kama Strakarnir okkar ikimaanisha wavuana wetu. Uwanja wake wa nyumbani ambao imekuwa ikiutumia kwa mechi za kimataifa unajulikana kama Laugardalsvoullur ulioko kwenye mji wa Reykjavik. Timu hii inaundwa na kikosi cha wachezaji wa chini ya umri wa miaka 21 ambao walifuzu kucheza fainali za mwaka 2011 kwenye ardhi ya Iceland.

Wakiongozwa na kocha wa muda mrefu wa Sweden, Lars Lagerback walimaliza kwenye nafasi pili kwenye kufuzu hatua ya makundi, ilikuwa ni kiwango bora zaidi ambacho kiliwahi kuoneshwa na timu hii wakati walipofuzu kucheza fainali za mwaka 2000.

Timu ya taifa ya Iceland imecheza jumla ya mechi 96, ikapata ushindi kwenye mechi 24, ikatoka sare mara 17, ikapoteza michezo 55, imefunga mabao 81 na kufungw amabao 146.

Timu ya taifa Ureno.

Matokeo mazuri ambayo timu ya taifa ya Ureno imewahi kuyarekodi ni kwa kumaliza kwenye nafasi ya pili kwenye michuano ya Ulaya ya mwaka 2004. Kikosi hiki kinanolewa na kocha mkuu Fernando Santos.

Mchezaji wa muda wote wa timu hii anayeongoza kwa kufunga mabao mengi akiwa na timu ya taifa ni Christiano Ronaldo aliyefunga mabao 55 rekodi ambayo anaishikilia hadi sasa.

Wachezaji wa muda wote waliocheza mechi nyingi zaidi wakiwa na timu ya taifa ya Ureno ni pamoja na Luis Figo aliyecheza mechi 127 na kwasasa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi ni Christian Ronaldo aliyecheza mechi 123.

Jina la utani la timu hii inafahamika kama Seleccao das Quinas, na imekuwa haina uwanja maalumu inapocheza mechi zake za kimataifa. Ureno ilifanikiwa kufika hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kombe la Ulaya iliyofanyika kwenye ardhi yake mwaka 2004 lakini ikapoteza mbele ya Ugiriki na kuwa timu nyingine kwenye ukanda wa Ulaya kupoteza mchezo wa fainali kwenye ardhi yake ya nyumbani.

Timu ya taifa ya Ureno imecheza mara mbili kwenye fainali za kombe la dunia la mwaka 2006 na kombe la Ulaya mwaka 2012 na kupoteza mchezo wake mbele ya Uhispania kwa njia ya matuta.

Kiujumla timu hii imecheza mechi 135, imeshinda mechi 76, ikatoka sare mara 29, imepoteza mechi 30, imefunga mabao 234 na kufungwa mara 127.

Timu hii ilishiriki kwa mara ya kwanza kwenye fainali za kombe la Ulaya mwaka 1984 na kucheza na Ufaransa kwenye hatua ya fainali kabla ya Michel Platin kuwamaliza kwa bao la ushindi.

Walifuzu tena kwenye fainali za mwaka 1996 na nimiongoni mwa mataifa 7 ya ukanda wa Ulaya yaliyocheza karibu kwenye fainali zote tano za kombe la Ulaya zilizopita sambamba na Uhispania, Ujerumani, Italia, Ufaransa, Uholanzi na Jamhuri ya Czech.

Timu ya taifa ya Ureno haijawahi kushindwa kuvuka hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Ulaya, na kushindwa kwenye hatua ya nusu fainali kwa mabingwa wa mwaka 1984 na 2000 Ufaransa na mwaka 2012 dhidi ya Uhispania.