EURO 2016

Hart: Uingereza itafika mbali michuano ya Ulaya

Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Uingereza, Joe Hart
Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Uingereza, Joe Hart Reuters / Hannah McKay Livepic

Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Uingereza, Joe Hart, anasema kuwa ni lazima timu yake "icheze kwa nguvu" ikiwa inataka kufika mbali kwenye michuano ya mwaka huu ya kombe la mataifa Ulaya ili kuwapa wakati mpya kizazi cha sasa kukumbuka historia ya mwaka 1996.

Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha kocha Roy Hodgson, ambacho kimeshinda kila mechi za kufuzu ilizocheza, itashuka uwanjani kucheza mchezo wake wa kwanza siku ya Jumamosi ambapo itapambana na Urusi, kwenye mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Marseille.

Hart anasema kuwa "ikiwa tutakuwa kwenye hali nzuri kwa muda mrefu, basi tutamaliza tukiwa na furaha." alisema mlinda mlango huyo.

Mlinda mlango huyo wa klabu ya Manchester City, amesema pia safu ya ulinzi ya timu yake inamatarajio makubwa licha ya ukosolewaji kuwa timu hiyo haina upana wa kikosi cha kushindana kwenye michuano ya mwaka huu.

Joe Hart akizungumza na wanahabari, Paris
Joe Hart akizungumza na wanahabari, Paris REUTERS/Lee Smith

Kikosi cha wachezaji 23 wa Uingereza kimesheheni wachezaji wengi ambao ni vijana, ambapo safu ya ulinzi itaongozwa na gary Cahill, Chris Smalling na John Stones, huku kiungo Eric Dier akiwa kama mlinzi wa akiba.

Joe Hart anasema kuwa anaamini kikosi chake ni cha wastani na chenye uwiano mkubwa, na kwamba mabeki waliochaguliwa, wana uwezo mkubwa wa kuhakikisha washambuliaji wa timu pinzani hawapati nafasi ya kufunga.

Hart ambaye kwa sasa ameichezea timu yake ya taifa mechi 59, alikuwa chaguo la kwanza kwenye fainali za kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil, ambapo waliondolewa kwenye hatua ya makundi.