EURO 2016

Wajue vijana 10 wanaotarajiwa kung'ara kombe la Ulaya 2016

Marcus Rashford, mchambuliaji kinda wa timu ya taifa Uingereza
Marcus Rashford, mchambuliaji kinda wa timu ya taifa Uingereza Reuters / Ed Sykes Livepic

Moja ya mambo yanayotazamwa sana kwenye michuano ya kimataifa ni kutazama vipaji vipya vinavyoibuka katika soka na kuonesha uwezo kwenye jukwaa la michezo, na michuano ya kombe la mataifa Ulaya mwaka huu, inayofanyika nchini Ufaransa inatarajiwa kutoa vijana wenye umri mdogo wakitafuta nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza. 

Matangazo ya kibiashara

Watu kama Kingsley Coman na Marcus Rashford, majina yao yanaweza yasiwe mageni kwenye masikio na macho ya wapenda soka, shukrani kwa klabu zao zilizoamua kuwapa nafasi kuonekana, mashindano ya mwaka huu ya kombe la Ulaya yatashuhudia vijana wenye umri mdogo zaidi ya kumi wakipata nafasi zao za kwanza kucheza mechi za kimataifa.

Jambo la kufurahisha mwaka huu ni kuwa kati ya vijana kumi walioambatana na timu zao, wachezaji watatu wanatoka kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uswis, na watakuwa na kazi ya kufikia mafanikio aliyoya[ata mwenzao, Johan Vonlanthen aliyewavutia watu wengi kwenye michuano ya mwaka 2004 aliyekuwa kijana mwenye umri wa miaka 18 na siku 137.

Wachezaji hao ni kama ifuatavyo:

Jina: Ante Coric, timu ya taifa ya Croatia.

Ante Coric, kiubgo wa timu ya taifa ya Croatia
Ante Coric, kiubgo wa timu ya taifa ya Croatia REUTERS/John Sibley

Umri: Miaka 19.
Nafasi anayocheza: Kiungo
Klabu: Dinamo Zagreb
Mafanikio: Amekuwa mchezaji wa nne kijana zaidi kufunga goli kwenye historia ya michuano ya UEFA Europa League, wakati alipofunga bao kwenye mechi kati ya timu yake na Astra Giurgiu akiwa na miaka 17 na siku 157, hii ilikuwa ni September, mwaka 2014.

 

 

 

Jina: Marcus Rashford, timu ya taifa Uingereza.

Marcus Rashford, mchambuliaji kinda wa timu ya taifa Uingereza
Marcus Rashford, mchambuliaji kinda wa timu ya taifa Uingereza REUTERS/John Sibley

Umri: Miaka 18.
Nafasi anayocheza: Mshambuliaji
Klabu: Manchester United.
Mafanikio: Aliingia dakika za mwisho kuchukua nafasi ya Anthony Martial na kufunga mabao 2 katika mechi yake ya kwanza kwenye kikosi cha United.

 

 

 

 

 

Jina: Kingsley Coman, timu ya taifa Ufaransa.

Kingsley Coman, mshambuliaji kinda wa timu ya taifa Ufaransa
Kingsley Coman, mshambuliaji kinda wa timu ya taifa Ufaransa REUTERS/Vincent Kessler

Umri: Miaka 19
Nafasi anayocheza: Mshambuliaji
Klabu: Beyern Munich na yuko kwa mkopo akitokea Juventus.
Mafanikio: Ameshinda nafasi ya pili ya michuano ya klabu bingwa Ulaya akiwa na klabu yake ya Juventus, akifunga bao na kuisaidia timu yake.

 

 

 

 

 

Jina: Bartosz Kapustka, timu ya taifa Poland.
Umri: Miaka 19.
Nafasi anayocheza: Kiungo
Klabu: Cracovia.
Mafanikio: Alifunga bao katika dakika ya 11 akiichezea timu yake ya taifa mwezi September mwaka jana.

Jina: Renato Sanches, timu ya taifa Ureno.

Renato Sanchez, kiungo wa timu ya taifa ya Ureno
Renato Sanchez, kiungo wa timu ya taifa ya Ureno REUTERS/Rafael Marchante

Umri: Miaka 18.
Nafasi anayocheza: Kiungo
Klabu: Bayern Munich
Mafanikio: Alijipatia umaarufu baada ya kuachia shuti kali akiwa mita 30 na kufunga bao lililoisaidia timu yake ya Benfica kuifunga Académica.

 

 

 

 

 

Jina: Nico Elvedi, timu ya taifa Uswis.

Nico Elvedi beki wa kati kinda timu ya taifa Uswis
Nico Elvedi beki wa kati kinda timu ya taifa Uswis REUTERS/Rafael Marchante

Umri: Miaka 19.
Nafasi anayocheza: Beki
Klabu: Mönchengladbach
Mafanikio: Aliitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Uswisi kushiriki fainali za kombe la Ulaya mwaka huu, siku mbili tu baada ya kupata nafasi kwenye mchezo dhidi ya Ubelgiji, akipewa nafasi ya mkongwe Philippe Senderos.

 

 

 

 

Jina: Denis Zakaria, timu ya taifa Uswis.

Denis Zackaria, kiungo kinda timu ya taifa Uswis
Denis Zackaria, kiungo kinda timu ya taifa Uswis uefa.com

Umri: Miaka 19.
Nafasi anayocheza: Kiungo.
Klabu: Young Boys.
Mafanikio: Alipata nafasi kwa mara ya kwanza kwenye timu ya taifa wakati ilipocheza na Ubelgiji kwenye mchezo wa kirafiki mwezi uliopita, akifunga bao lake la kwanza wakati klabu yake ya Young Boys ilipoifunga St Gallen, 2-1.

 

 

 

Jina: Breel Embolo, timu ya taifa Uswis.

Breel Embolo mchambuliaji kinda wa timu ya taifa Uswis
Breel Embolo mchambuliaji kinda wa timu ya taifa Uswis REUTERS/Arnd Wiegmann

Umri: Miaka 19.
Nafasi anayocheza: Mshambuliaji.
Klabu: FC Basel.
Mafanikio: Anakuwa mchezaji wa sita kwenye historia ya UEFA kucheza mechi za klabu bingwa Ulaya wakati alipofunga bao la kwanza la timu yake dhidi ya Ludogorets, mwezi November mwaka 2014.

 

 

 

  

Jina: Emre Mor, timu ya taifa Uturuki.

Emre Mor, mshambuliaji wa timu ya taifa Uturuki
Emre Mor, mshambuliaji wa timu ya taifa Uturuki

Umri: Miaka 18.
Nafasi anayocheza: Mshambuliaji.
Klabu: Nordsjælland.
Mafanikio: Anafanishwa na Lionel Messi kwa aina ya mchezo na namna anavyoumiliki mpira, aliifungua timu yake bao la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Kobenhavn, mwezi March, mwaka huu.

 

 

 

 

Jina: Olexandr Zinchenko, timu ya taifa Ukraine.

Olexandre Zinchenko kiungo kinda wa timu ya taifa Ukraine
Olexandre Zinchenko kiungo kinda wa timu ya taifa Ukraine REUTERS/Rafael Marchante

Umri: Miaka 19.
Nafasi anayocheza: Kiungo.
Klabu: Ufa.
Mafanikio: Alivunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Andriy Shevchenko, akiwa ni mchezaji kinda kwenye timu ya taifa ya Ukraine, akifunga goli dhidi ya Romania ikiwa ni mara yake ya pili kucheza May 29