OSCAR PISTORIUS - AFRIKA KUSINI

Baba wa Reeva, ataka Pistorius alipe kifo cha mwanae

Baba mzazi wa mwanamitindo, Reeva Steenkamp, aliyeuawa na mchumba wake Oscar Pistorius usiku wa kuamkia siku ya wapenda nao, ameangua kilio mahakamani wakati akitoa ushahidi

Baba mzazi wa marehemu Reeva Steenkamp, akiwa mahakamani 13June2016
Baba mzazi wa marehemu Reeva Steenkamp, akiwa mahakamani 13June2016 REUTERS/Phill Magakoe/Pool
Matangazo ya kibiashara

Akiwa kizimbani, Barry, ameiambia mahakama kuwa mwanariadha huyo ni lazima alipe gharama ya kifo cha mwanawe na ni kwakupewa adhabu anayostahili kutokana na kosa lenyewe alilolifanya.

Barry amesema kuwa "Imekuwa ngumu sana kwake kusamehe...nahisi Oscar ni lazima alipe kutokana na alichokifanya, lazima alipe kutokana na kosa la mauaji." Alisema Barry Steenkamp mwenye umri wa miaka 73.

Mahakama kuu ya Afrika Kusini inasikiliza upya kesi dhidi ya mwanariadha huyo na kutoa hukumu mpya dhidi yake, baada ya mahakama ya rufaa kutengua hukumu ya awali ambayo ilitolewa kimakosa kwa misingi ya sheria.

Oscar Pistorius akiwa mahakamani siku ya Jumatatu, June 13
Oscar Pistorius akiwa mahakamani siku ya Jumatatu, June 13 REUTERS/Mike Hutchings/Files

Kwa msingi huo sasa wataalamu wa sheria nchini Afrika Kusini, wanasema kuwa uamuzi wa mahakama ya rufaa ni kuwa Oscar Pistorius ashtakiwe kwa kosa la mauaji, kosa ambalo kwa sheria za Afrika Kusini, kifungo cha chini ni miaka 15.

Mwezi Machi mwaka huu, mawakili wa Pistorius walishindwa kutengua uamuzi wa awali wa mahakama ya rufaa iliyotaka mteja wao ashatakiwe kwa kosa la kuua kwa kukusudia.

Baba wa Reeva, ameiambia mahakama kuwa yeye anaamini kabisa pasipo na shaka, ya kwamba mwanae na mchumba wake waligombana usiku wa kuamkia siku yenyewe ya wapendanao.

Mwanariadha Oscar Pistorius anasisitiza kuwa alimfyatulia mchumba wake risasi akiwa chooni akidhania kuwa nyumba yake ilikuwa imevamiwa na majambazi, utetezi ambao mwendesha mashtaka wa Serikali anaupinga kwa nguvu zote.