NBA - MAREKANI

Fainali NBA: Cavaliers yaifunga Worriors kwenye mchezo wa 5

Mchezaji wa Cleveland cavaliers, LeBron James
Mchezaji wa Cleveland cavaliers, LeBron James Cary Edmondson-USA TODAY Sports

Timu ya mpira wa kikapu ya Cleveland Cavaliers imeifunga timu ya Golden State Worriors kwa vikapu 112 kwa 97 na kupunguza alama hadi kufikia alama 3-2 katika timu 7 bora kutinga fainali za ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani, NBA. 

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa LeBron james na Kyrie Irving, kila mmoja amefanikiwa kufunga alama 41 na kuwa wachezaji wa kwanza kutoka timu moja, kufunga zaidi ya alama 40 kwenye mchezo mmoja wa fainali ya NBA.

Steph Curry alifunga alama 25 pekee huku Worriors wakimkosa mchezaji wao anayetumikia adhabu, Draymond Green, wakati waliposhindwa kuchukua ubingwa wakiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Timu ya Worriors inarejea kwenye uwanja wa Cleveland ambako walishinda taji la mwaka 2015, katika michezo sita.

Mchezaji wa Golden State Worriors, Stephen Curry
Mchezaji wa Golden State Worriors, Stephen Curry Kelley L Cox-USA TODAY Sports

Hakuna timu yoyote iliyoweza kurejea kutoka kwenye alama 3-1 ilizopoteza na kushinda kwenye fainali, lakini Cavaliers wanahisi kama sasa wanao uwezo na nia ya kufanya vizuri kwenye uwanja wake wa nyumbani siku ya Alhamisi na kuamuliwa tena siku ya Jumapili kujua nani mshindi.

Cleveland walipata alama 10 kati ya 20 za alama tatu na kuifaya timu ya Worriors kuangukia pua kwa mara ya nne kwenye uwanja wake wa nyumbani msimu huu.

Matokeo yalikuwa alama sawa 61 kwa 61 wakati wa mapumziko, lakini Cleveland walirejea kwa nguvu na kupata vikapu 51 kwa 36, huku Curry akishindwa kufurukuta katika timu kwa kufunga alama 21 kwa mitupo ya alama tatu.

Kwa sasa ni mara ya 26 mfululizo kwa mchezaji LeBron James kushinda taji jingine kutengeneza rekodi yake kwenye mashindano ya NBA.