EURO 2016

Urusi kutupwa nje kombe la Ulaya 2016, mashabiki wake waonywa

Wafanyakazi wa Uefa wakitandaza uwanjani moja ya bango la shirikisho la mpira Ulaya
Wafanyakazi wa Uefa wakitandaza uwanjani moja ya bango la shirikisho la mpira Ulaya REUTERS/Regis Duvignau Livepic

Nchi ya Urusi huenda ikaondolewa kwenye michuano ya kombe la Ulaya 2016, ikiwa mashabiki wake watajihusisha kwenye vurugu nyingine katia mechi zilizosalia za timu hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umechukuliwa baada ya kukamilika kwa kikao cha nidhamu cha kamati ya shirikisho la mpira Ulaya, UEFA, kamati ambayo imeamua kuipa adhabu ya kulipa faini na kuitoa ikiwa mashabiki wake watahusika kwenye vurugu zaidi.

Uefa pia imeipiga nchi ya Urusi, faini ya paundi za Uingereza laki 1 na elfu 20, kutokana na vurugu za mwishoni mwa juma wakati timu yao ilipomaliza kucheza na timu ya taifa ya Uingereza, mjin Marseille.

Urusi pia imejikuta matatani baada ya mashabiki wake kubainika kuwa walitoa matamshi ya kibaguzi na kuwasha fataki wakati wa mchezo, vitendo ambavyo vimeenda kinyume na kanuni za mashindano ya mwaka huu.

Mashabiki wa soka wa Urusi wakikabiliana na wale wa Uingereza
Mashabiki wa soka wa Urusi wakikabiliana na wale wa Uingereza Reuters/路透社

Katika hatua nyingine, kundi la mashabiki wa Urusi, liko mbioni kurudishwa nchini mwao kutoka Ufaransa baada ya kujirudia kwa matukio ya uvunjifu wa amani.

Adhabu ya iliyoahirishwa kwa muda ya kutupwa nje ya michuano ya mwaka huu sambamba na kulipa faini, imehusisha matukio pekee yaliyojitokeza mwishoni mwa juma lililopita, na kwamba Uefa iko wazi ikiwa Urusi itakata rufaa.

Hata hivyo waziri wa michezo wa Urusi na rais wa shirikisho la kabumbu nchini humo, Vitaly Mutko, amesema Urusi itaheshimu uamuzi wa Uefa na kuhoji, je ni suala gani jingine linaweza kufanywa? alimaliza rais huyo.