LIGI KUU UINGEREZA

Ratiba ya ligi kuu Uingereza yatolewa

Mpira unaotumiwa kwenye ligi kuu ya Uingereza
Mpira unaotumiwa kwenye ligi kuu ya Uingereza Reuters/Carl Recine/File Photo

Chama cha soka nchini Uingereza hatimaye kimeweka wazi ratiba ya msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini humo, inayotarajiwa kuanza August 13, kwa mabingwa Leicester City kuwakaribisha Hull City iliyopanda daraja.

Matangazo ya kibiashara

Mechi kubwa ya ufunguzi wa ligi hiyo, inatarajiwa kuikutanisha klabu ya Arsenal ambayo itakuwa mwenyeji wa vijogoo vya jiji, Liverpool.

Makocha waliopewa timu mpya msimu huu, kocha Jose Mourinho anayekinoa kikosi cha Manchester United, atakutana kwa mara ya kwanza na mpinzani wake aliyekuwa nae kwenye ligi ya Uhispania, Pep Guardiola ambaye msimu huu atakinoa kikosi cha Manchester City, timu hizi zitakutana kwenye dimba la Old Trafford, September 10.

Klabu wa West Ham ambayo ilihama uwanja wake wa awali na sasa itakuwa inatumia uwanja wake mpya wa Olympic, itakuwa nyumbani kuikaribisha klabu ya Bournemouth, August 20.

RFI

Mambo muhimu ambayo yanatarajiwa kwenye ligi kuu ya msimu huu, ni pamoja kocha Jose Mourinho kukutana na kocha mpya wa Chelsea, Antonio Conte kwenye dimba la Stamford Bridge, October 22.

Mechi ya kwanza ya wapinzani wa jadi kwenye jiji la London, itapigwa November 5, ambapo Arsenal watakuwa nyumbani kuikaribisha klabu ya Tottenham Hotspurs, huku wapinzani wa jadi wa Merseyside, klabu ya Everton itakuwa nyumbani kuikaribisha Liverpool, December 17.

Kocha Jurgen Klopp ambaye aliwahi kufundisha ligi ya Ujerumani na kukutana mara kadhaa na aliyekuwa kocha wa Beyern Munich, Pepe Guardiola, watakutana kwa mara nyingine wakiwa na timu tofauti tarehe 1 January 2017, wakati Liverpool itakapoikaribisha Manchester City.

Kwa ratiba kamili ya mechi zote za ligi kuu ya Uingereza, bofya hapa.

Ratiba fupi ya mechi za Ufunguzi:

13 AUGUST :

Arsenal v Liverpool

Bournemouth v Manchester United

Burnley v Swansea City

Chelsea v West Ham United

Crystal Palace v West Bromwich Albion

Everton v Tottenham Hotspur

Hull City v Leicester City

Manchester City v Sunderland

Middlesbrough v Stoke City

Southampton v Watford

 

MECHI ZA MWISHO:

21 MAY;

Arsenal v Everton

Burnley v West Ham United

Chelsea v Sunderland

Hull City v Tottenham Hotspur

Leicester City v Bournemouth

Liverpool v Middlesbrough

Manchester United v Crystal Palace

Southampton v Stoke City

Swansea City v West Bromwich Albion

Watford v Manchester City