CAF

Vlabu vya soka barani Afrika vyaingia kwenye mapambano

cafonline

Michuano ya soka hatua ya makundi, kuwani taji la klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika inaanza kutifua vumbi leo Jumamosi katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Michuano hii inachezwa nyumbani na ugenini kutafuta bingwa.

Taji la klabu bingwa, lina vlabu nane, katika makundi mawili, kila kundi na timu nne sawa na lile la Shirikisho.

RATIBA YA KLABU BINGWA

Jumamosi Juni 18 2016
Zesco United (Zambia) vs Al Alhly(Misri)-Saa 10 na nusu

ASEC Mimosas (Cote Dvoire) vs Wydad Casablanca (Morocco)- Saa Moja na nusu

ES Setif (Algeria) vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)- Saa Sita na dakika 15 usiku.

Uchambuzi muhimu:-

Mabingwa wa Misri Al Ahly, wanarejea katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza ndani ya miaka miwili katika michuano hii.

Wamenyakua taji hili mara nane katika historia yake ya kushiriki katika michuano hii.

Hata hivyo, Al Ahly inacheza mechi hii bila ya wachezaji wake wa kutegemewa kama Abdullah El Said, Malick Evouna na Amr Gama ambao wamejeruhiwa.

Zesco United inayoshiriki katika hatua hii ya makundi iko nyumbani mjini Ndola.

Wydad Casablanca ambayo iliiondoa TP Mazembe ya DRC katika hatua ya mwondoano,wapo ugenini kumenyana na ASEC Mimosas.

Mwaka 2011, katika michuano hii, Wydad Casablanca walimaliza katika nafasi ya pili.

Kuelekea katika hatua hii ya makundi, Asec Mimosas imekuwa ikijaribu kuimarisha kikosi chake kwa kumsajili mchezaji Yahaya Mohammed raia wa Ghana anayechezea klabu ya Aduana Stars, bila mafanikio.

Mamelodi Sundowns nao wanachuana katika hatua hii baada ya kufungiwa kwa AS Vita Club ya DRC kwa kumchezesha mchezaji ambaye alikuwa amefungiwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Jumapili Juni 19 2016
Enyimba (Nigeria) vs Zamalek(Misri) -Saa 12 jioni

RATIBA YA TAJI LA SHIRIKISHO.

Matokeo Jumamosi
Kawkab Marrakech (Morroco) 2 vs Etoile du Sahel (Tunisia) 1

Jumapili Juni 19 2016
TP Mazembe (DRC) vs Medeama (Ghana) – Saa kumi na dakika 30
MO Bejaia (Algeria) vs Yanga FC (Tanzania) – Saa sita na dakika 15

Jumatatu Juni 20 2016
FUS Rabat(Morroco) vs Al Ahli Tripoli (Libya)- Saa saba kamili usiku

Maelezo muhimu:
Klabu ya Medeama inaamini kuwa inaweza kufanya vizuri katika michuano hii na hata kuishinda TP Mazembe mjini Lubumbashi pamoja na changamoto nyingi za kifedha.

Hivi karibuni kumekuwa na wasiwasi kuhusu ushiriki wa klabu hii ya Ghana, katika michuano hii.

Moses Armah rais wa klabu hii, amesema vijana wake wamejiandaa kisaikolojia kushinda mechi yao ya kwanza na hatimaye kunyakua taji hili ili kujipatia kitita cha Dola za Marekani 150,000.

Yanga ya Tanzania nayo ilikuwa imepiga kambi nchini Uturuki, kujiweka tayari kwa michuano hii hasa mechi yake ya kwanza dhidi ya MO Bejaia.

Klabu hii ya Tanzania imeweka historia kwa kufika katika hatua hii ya makundi, pamoja na kibarua kigumu kinachowasubiri.