EURO 2016

Ufaransa kutafuta ushindi mechi ya mwisho kundi A

Uwanja wa soka wa Saint-Denis jijini Paris
Uwanja wa soka wa Saint-Denis jijini Paris UEFA Photos

Michuano ya soka kuwania ubingwa wa bara Ulaya inaendelea nchini Ufaransa na leo Jumapili, ni mechi za kutamatisha kundi A.

Matangazo ya kibiashara

Mchuano uliopita Ufaransa na Albania
Mchuano uliopita Ufaransa na Albania UEFA Photos

Mechi hizi zinachezwa kwa muda sawa, kuanzia saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.

Wenyeji Ufaransa watachuana na Uswizi, huku Romania wakimenyana na Albania.

Ufaransa wanaongoza kundi hili kwa alama 6, Uswizi ni ya pili kwa alama 4, Romania ni wa tatu huku Albania wakiwa ya mwisho.

Wachezaji wa Uswizi wakifanya mazoezi
Wachezaji wa Uswizi wakifanya mazoezi UEFA Photos

Kesho ni mechi za kundi B, Urusi watachuana na Wales , lakini Slovakia watachuana na Uingereza.

Baada ya kumalizika kwa michuano ya makundi, mataifa 16 yatafuzu katika hatua ya mwondoano.

Italia tayari imeshafuzu katika hatua hii na inasubiri mshindi wa pili katika kundi D.

Siku ya Jumamosi, Iceland ilitoka sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya Hungary, huku Ureno nayo ilikitoka sare ya kutofungana na Austria.