NBA-MAREKANI

LeBron aibeba Cavaliers kushinda taji na kuweka historia

Wachezaji na viongozi wa timu ya Cavaliers wakishangilia ushindi wa taji lao la kwanza la NBA.
Wachezaji na viongozi wa timu ya Cavaliers wakishangilia ushindi wa taji lao la kwanza la NBA. Cary Edmondson-USA TODAY Sports

Timu ya mpira wa kikapu ya Cleveland Cavaliers imefanikiwa kuweka historia kwenye fainali ya michuano ya ligi ya kikapu ya Marekani, NBA, baada ya kuifunga Golden State Warriors kwa alama 93-89. 

Matangazo ya kibiashara

Nchezaji wa Cavaliers, LeBron James aliiongoza timu yake kuweka historia hiyo baada ya kurejea toka kwenyeh mechi tatu za awali walizokuwa wamefungwa, na kutengeneza historia kwenye mchezo wa saba uliotoa bingwa mpya kwa staili ambayo wengi hawakutarajia.

Hili linakuwa ni taji la kwanza kwa timu ya Cleveland Cavaliers kushinda.

Ushindi dhidik ya Warriors, ambao waliwafunga Cleveland kwenye fainali ya mwaka jana, inakuwa timu ya kwanza kufanikiwa kushinda taji hili kutoka kupoteza michezo mitatu ya awali na kushinda kwenye mchezo wake wa saba, kushinda taji la NBA.

"Nimekuwa na ndoto hii kwa zaidi ya miaka miwili toka nijee ili kuleta taji kwenye mjik huu," alisema LeBron ambaye alikuwa akilia kutokana na kutoamini ushindi iliyoupata timu yake.

Mchezaji wa Cleveland Cavaliers, LeBron James akiwa na vikombe alivyoshinda sambamba na timu yake.
Mchezaji wa Cleveland Cavaliers, LeBron James akiwa na vikombe alivyoshinda sambamba na timu yake. Bob Donnan-USA TODAY Sports

LeBron alirejea kuichezea Cleveland mwaka 2014 baada ya kutumia miaka minne akiwa na timu ya Miami Heat, ambapo pia akiwa na timu hiyo alifanikiwa kutwaa nayo taji la NBA kwenye fainali.

LeBron anasema "Nilitoa kila kitu nilichokuwa nacho. Niliweka moyo wangu, damu, jasho na machozi yangu kwenye mchezo huu." alisema mchezaji huyo.

LeBron aliiongoza timu yake kupata taji la mwaka huu baada ya kufunga alama nyingi zaidi kwenye mchezo mmoja, ambapo usiku wa kuamkia leo alifunga alama 27, huku akipata ribaundi 11 na kusaidia wenzake kufunga mara 11, ushindi ambao pia umemfanya atajwe kama mchezaji mwenye thamani zaidi kwenye mchezo wa fainali, tuzo inayofahamika kama MVP.

Ushindi huu unamaliza miongo kadhaa ya ukame wa mataji kwa jiji la Cleveland, ambalo halijawahi kushinda taji kubwa la NBA toka mwaka 1964 katika ligi ya taifa ambayo imewahik kushiriki.

Kwa mchezaji LeBron, kushinda taji hili kunaweka ishara kwake kwa kufanikiwa kutwaa taji la tatu la NBA, lakini litakuwa ni historia kwake binafsi kama mchezaji aliyepata mafanikio zaidi na kutimiza ahadi kwa wakazi wa mji wake kuwa angefanikisha mji huo kutwaa taji.

Timu hii wakatik ikikabiliwa kuondoshwa kwenye mechi zake mbili zilizopita, LeBron aliibeba Cavaliers na kurejea kwenye mchezo, na kuifanya kuwa timu ya tatu kulazimisha fainali ya mwaka huu kuamuliwa kwenye mchezo wa saba.

Kwa timu ya Warriors, ambayo imeweka rekodi ya kucheza mechi 73 bila kupoteza kati ya michezo 82 ya msimu wa kawaida, kipigo cha kuamkia leo kinakuwa ni kipigo cha kwanza toka mwaka 2013 wakipoteza mechi tatu mfululizo.