CAF

Zesco United yaiangusha Al Ahly, Yanga yalemewa ugenini

cafonline

Zesco United ya Zambia ndio klabu pekee iliyopata ushindi nyumbani katika michuano ya kwanza ya hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, mechi zilizoanza mwishoni mwa juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa mara nane wa michuano hii, Al Ahly ya Misri walishindwa kuonesha ubabe wao katika uwanja wa Kimataifa wa Levy Mwanawasa mjini Ndola baada ya kufungwa na vijana wa nyumbani ZESCO United mabao 3 kwa 2.

Hata hivyo, klabu nyingine ya Misri Zamalek FC walijizatiti na kuanza kwa ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya mabingwa mara mbili wa taji hili Enyimba ya Nigeria mjini Port Harcourt.

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wakiwa ugenini nchini Algeria, waliwashinda Entente Setif ya Algeria mabao 2 kwa 0, huku Wydad Casablanca ya Morroco wakiwashinda Asec Mimosas ya Cote dvoire bao 1 kwa 0.

Wachezaji wa Mamelodi Sundowns wakisheherekea ushindi
Wachezaji wa Mamelodi Sundowns wakisheherekea ushindi Mamelodi photos

Mchuano dhidi ya Entente Setif na Mamelodi Sundowns ulitishwa kwa muda baada ya mashabiki wa nyumbani kuanza kurusha fataki uwanjani kuelekea mwisho wa mchuano huo na sasa klabu hiyo inasubiri kauli ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF ambayo huenda ikatangaza adhabu.

Matokeo kamili

Kundi A

Zesco United 3-2 Al Ahly

Asec Mimosas 0-1 Wydad Casablanca

Kundi B

Entente Setif 0-2 Mamelodi Sundowns
Enyimba 0-1 Zamalek

Baada ya michuano hiyo ya mwisho mwa juma lililopita, hivi ndivyo jedwali la makundi lilivyo.

Kundi A
1.Zesco United -3
2.Wydad Casablanca-3
3.Al-Ahly-0
4.ASEC Mimosas-0

Kundi B
1.Mamelodi Sundowns- 3
2.Zamalek-3
3.Enyimba-0
4.ES Setif-0

Mechi zijazo

Juni 28  2016
Al-Ahly vs ASEC Mimosas

Juni 29 2016

Mamelodi Sundowns vs Enyimba
Zamalek vs ES Setif
Wydad Casablanca vs Zesco United

Wachezaji wa TP Mazembe wakisherehekea ushindi
Wachezaji wa TP Mazembe wakisherehekea ushindi AFP PHOTO / STR

Michuano ya Shirikisho nayo, ilipigwa mwishoni mwa wiki iliyopita na timu zote zilizokuwa nyumbani zilipata ushindi.

Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Congo, ilianza vema safari yao ya kutafuta ubingwa wa taji hili kwa kupata ushindi wa mabao 3 kwa 1, dhidi ya klabu ya Medeama ya Ghana.

Mchuano huu ulichezwa katika uwanja wa Kamalondo mjini Lubumbashi na ni ushindi ambao umewapa matumaini mashabiki wa Mazembe k baada ya kuondolewa katika ile michuano ya klabu bingwa.

Rainford Kalaba mchezaji wa Kimataifa kutoka Zambia aliifungia klabu yake mabao mawili katika mchuano huo, huku bao lingine likitiwa kimyani na Salif Coulibaly.

Hata hivyo, Medeama ndio iliyoanza kupata bao katika dakika ya pili kupitia mchezaji wake Malik Akowuah.

Nayo Yanga FC ya Tanzania ikicheza ugenini nchini Algeria, ilifungwa bao 1 kwa 0 dhidi ya Mouloudia Bejaia.

Mabingwa watetezi wa taji hili Etoile du Sahel ya Tunisia walifungwa na Kawkab Marrakech ya Morocco mabao 2 kwa 1.

FUS Rabat ya Morroco nayo imeishinda Al Ahli Tripoli ya Libya kwa bao 1 kwa 0.

 

Kwa matokeo hayo:-

Kundi A

1.TP Mazembe -3
2.MO Bejaia-3
3.Yanga FC-0
4.Medeama-0

Kundi B
1.Kawkab Marrakech-3
2.FUS Rabat-3
3.Etoile du Sahel-0
4.Al-Ahli Tripoli-0

Mechi zingine zitachezwa mwishoni mwa mwezi huu
Juni 28 2016
Yanga vs TP Mazembe

Al-Ahli Tripoli vs Kawkab Marrakech

Juni 29 2016
Medeama vs MO Bejaia
Etoile du Sahel vs FUS Rabat