SOKA

Victor Wanyama ajiunga na Tottenham Hotspurs

Victor Wanyama, nahodha wa Harambee Stars
Victor Wanyama, nahodha wa Harambee Stars Kenya Dailypost

Nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars Victor Wanyama, amekamilisha usajili katika klabu ya Tottenham Hotspurs nchini Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Wanyama mwenye umri wa miaka 24 ambaye msimu uliopita aliichezea Southmptom FC, amesajiliwa katika klabu hii mpya kwa kiasi cha Pauni za Uingereza Milioni 11 na kutia saini mkataba wa miaka minne.

Kiungo huyo wa kati alikataa kuendelea kuichezea klabu yake ya zamani, baada ya Tottenham Hotspurs kuonesha nia ya kumsajili na atakutana tena na kocha wake wa zamani Mauricio Pochettino ambaye alikuwa kocha wake pia katika klabu ya Celtic huko Scotland.

Huu ndio usajili wa kwanza wa klabu ya hii ya Tottenham Hotspurs ambayo ilimaliza ya tatu msimu uliopita na inajiandaa ksuriki katika michuano ya kalbu bingwa barani Ulaya msimu ujao.

Wanyama amesema amefurahi sana kufanikiwa kujiunga na klabu hiyo na kuahidi kufanya bidii katika klabu hiyo baada ya kufanikiwa katika zoezi la upimaji afya.

“Ni ukurasa mpya katika maisha yangu na naahidi kutia bidii, lakini pia nawashukuru mashabiki wa Southmptom FC, kwa muda wote tuliokuwa pamoja,” alisema.

Wanyama anatarajiwa kurejea jijini Nairobi siku ya Jumatano kuendelea na likizo lake baada ya kufanikisha usajili huo.

Anasalia kuwa mchezaji peke kutoka ukanda wa Afrika Mashariki anayecheza soka la kulipwa katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza.