COSAFA

Namibia kusaka taji la kuwatuliza mashabiki wake

Mchezaji wa Namibia na Msumbiji wakipambana wiki iliyopita
Mchezaji wa Namibia na Msumbiji wakipambana wiki iliyopita Cosafa.com

Michuano ya soka kuwania taji la mataifa ya Kusini mwa Afrika COSAFA inaendelea leo nchini Namibia.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa yaliyopoteza michuano ya robo fainali, yanachuana katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la ngao katika michuano hii.

Lesotho watachuana na Zambia kuanzia saa 11 jioni saa za Afrika ya Kati, huku wenyeji Namibia wakitarajiwa kumenyana na Msumbiji.

Kesho Jumatano, kutakuwa na nusu fainali ya kuwania taji la mwaka huu.

Mechi ya kwanza itakuwa kati ya Afrika Kusini na Swaziland kuanzia saa 11 jioni huku, mechi ya pili ikiwa kati ya Botswana dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo saa moja na nusu saa za Afrika ya Kati.

Fainali ya michuano hii itachezwa siku ya Ijumaa, katika uwanja wa Sam Nujoma, jijini Windhoek.

Mfungaji bora hadi katika hatua hii ni Felix Badenhorst kutoka Swaziland.