RIADHA

Mashindano ya riadha ya barani Afrika yaanza Afrika Kusini

Uwanja wa riadha wa Kings Park nchini Afrika Kusini
Uwanja wa riadha wa Kings Park nchini Afrika Kusini Neville Bailey

Makala ya 20 ya mashindano ya riadha barani Afrika, inaanza leo Jumatano hadi Jumapili katika uwanja wa Kings Park, mjini Durban nchini Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Haya ni mashindano yanayowaleta pamoja wanariadha mbalimbali barani Afrika kutafuta ubingwa katika nyanja mbalimbali.

Aidha, ni mashindano yanayotumiwa na wanariadha wengi kujiweka tayari kwa michezo ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mwezi Agosti.

Mabingwa wa riadha barani Afrika, Kenya imetuma wanariadha 69 kushiriki katika mashindano haya chini ya kocha Samson Kitur.

Hii ndio idadi kubwa ya wanariadha wa nchi hiyo kuwahi kushiriki katika historia ya mashindano haya.

Wanariadha kutoka Kenya
Wanariadha kutoka Kenya IAAF

Mataifa mengine yaliyotoa wanariadha wengi ni pamoja na Nigeria na wenyeji Afrika Kusini.

Siku ya kwanza, michezo inayoshuhudiwa ni ile ya kurusha kitufe, shot put kwa wanaume na wanawake, kuruka na mbio fupi za mita 100, 400.

Mataifa karibu yote ya bara Afrika yanashiriki katika mashindano haya, yakiwemo mataifa yote ya Afrika Mashariki ni kati ambayo ni pamoja na Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.