URENO-HUNGARY-EURO 2016

Ureno yatinga katika mzunguko wa nane

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Ureno, Cristiano Ronaldo, aliyefunga mabao mawili dhidi ya Hungary katika michuano ya Kombe la Ulaya, Lyon.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Ureno, Cristiano Ronaldo, aliyefunga mabao mawili dhidi ya Hungary katika michuano ya Kombe la Ulaya, Lyon. AFP

Michuano ya Kombe la Ulaya inayoendelea kupigwa katika viwanja mbalimbali vya soka nchini Ufaransa. Jumatano hii Juni 22 Ureno wamefuzu katika mzunguko wa nane katika michuano ya Kombe la Ulaya (Euro 2016) kwa kutoka sare dhidi ya Hungary ya kufungana mabao (3-3).

Matangazo ya kibiashara

Mabao mawili ya Ureno yamewekwa kimyani na nyota wake Cristiano Ronaldo.

Ureno itamenyana na Croatia katika mechi ijayo, itakayopigwa Jumamosi Juni 25 katika uwanaja wa Lens.

Wakifungwa mabao matatu mfululizo baada ya Gera kuweka kimyani bao la kwanza katika dakika ya 19 na Dzsudzsak aliyefunga mabao mawili peke yake katika dakika ya 47na 55, vijana wa Fernando Santos walisawazisha kupitia mchezaji Nani aliyeifungia timu yake bao la kwanza na kupunguza matokeo katika dakika ya 42 pamoja na Cristiano Ronaldo aliyefanikiwa kuliona lango la Hungary mara mbili katika dakika ya 50, 62.

Ureno inamaliza ikiwa nafasi ya tatu katika Kundi F. Hungary wanamaliza wakiwa wa kwanza katika kundi hilo mbele ya Iceland na watatasubiri matokeo ya Kundi E ili kutambua timu watakayomenyana nayo siku zijazo.

Ronaldo ametokea kuwa mchezaji wa kwanza katika historia kwa kufunga katika michuano tofauti ya Kombe la Ulaya, akiwa na jumla ya mabao 8 katika hatua ya fainali, akiongoza kwa rekodi mbele ya Platini.