RIADHA

Stephen Mokoka ashinda mbio za Mita 10 000

Mwanariadha wa Afrika Kusini Stephen Mokoka
Mwanariadha wa Afrika Kusini Stephen Mokoka citizen.co.za

Mashindano ya riadha ya bara Afrika yanaendelea kwa siku ya pili leo Alhamisi mjini Durban nchini Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Fainali ya ya Mita 5000 kwa upande wa wanawake, zinasubiriwa jioni ambapo wanariadha kutoka Afrika Mashariki watapambana.

Wanariadha hao watajaribu kuvunja rekodi ya mwanariadha Tirunesh Dibaba kutoka Ethiopia, aliyeweka rekodi katika mbio hizo mwaka 2008 kwa kuweka muda wa dakika 14 na sekunde 11.

Siku ya Ijumaa, kutakuwa na fainaili ya mbio za Mita 800 kwa upande wa wanaume, pamoja na Mita 3000 kuruka viunzi na maji.

Fainali ya Mita 1500 kwa upande wa wanawake pia itafanyika kesho.

Wenyeji Afrika Kusini walianza vema baada ya kushinda medali mbili za dhahabu.

Mwanariadha Stephen Mokoka aliweka historia kwa kuwapa raha mashabiki wa nyumbani baada ya kushinda mbio za Mita 10,000 kwa upande wa wanaume kwa kutumia muda wa dakika 28, dakika 2 na sekunde 97.

Mkenya Wilfred Kimitei alimaliza katika nafasi ya pili kwa muda wa saa 28:03.18.

Mashindano hayo yanatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii.