SOKA

Urusi 2018: Droo ya mataifa ya Afrika kufuzu kombe la dunia yawekwa wazi

Safari ya mataifa ya Afrika, kufuzu katika michuano ya soka ya kombe la dunia mwaka 2018 imefikia katika hatua ya lala salama baada ya Shirikisho la soka barani Afrika kufanya droo ya hatua ya makundi siku ya Ijumaa. 

Matangazo ya kibiashara

Droo hiyo ilifanyika katika makao makuu ya CAF jijini Cairo nchini Misri na hivi ndivyo mataifa hayo 20 yalivyopangwa katika makundi matano:-

Kundi A Libya, Guinea, DR Congo na Tunisia.

Kundi B Cameroon, Zambia, Nigeria na Algeria.

Kundi C Gabon, Morocco, Mali na Ivory Coast

Kundi D Burkina Faso, Afrika Kusini, Cape Verde na Senegal,

kundi E  Uganda, Misri, Congo na Ghana

Michuano hii ya makundi itachezwa nyumbani na ugenini kati ya mwezi Oktoba mwaka huu na Novemba mwaka 2017.

Mshindi wa kila kundi, atakayepata alama nyingi baada ya mechi zote kukamilika, atafuzu katika fainali hiyo na kufanya bara la Afrika kuwa na mataifa yatakayokwenda Urusi.

Cameroon inashikilia rekodi ya kufuzu katika michuano hii mara nyingi zaidi miongoni mwa mataifa ya Afrika, baada ya kufuzu mara 7 mwaka 1982, 1990, 1994, 1998, 2002, 2010 na 2014.

Nigeria nayo imefuzu mara tano, mwaka 1994, 1998, 2002, 2010 na 2014.
Mataifa mengine ambayo yamewahi kufuzu ni pamoja na Algeria, Morroco na Tunisia zote mara 4.

Cote Dvoire, Ghana, Afrika Kusini mara 3, Misri mara 2 huku Zaire( DRC), Senegal, Angola na Togo zikifuzu mara 1.