RIADHA

Afrika Kusini yamaliza ya kwanza katika mashindano ya bara Afrika

Wanariadha wa Afrika Kusini baada ya kupata ushindi katika mbio fupi
Wanariadha wa Afrika Kusini baada ya kupata ushindi katika mbio fupi athletics-africa.com

Afrika Kusini imemaliza ya kwanza katika mashindano ya bara Afrika yaliyomalizika jana mjini Durban.

Matangazo ya kibiashara

Wenyeji wa mashindano hayo walimaliza katika nafasi hiyo baada ya kupata medali 33, ikiwemo 16 za dhahabu.

Mabingwa wa riadha kutoka Afrika Mashariki Kenya, walimaliza katika nafasi ya pili baada ya kujinyakulia medali 24, zikiwemo 8 dhahabu.

Hata hivyo, uongozi wa Shirikisho la riadha barani Afrika umeonya kuwa mataifa ambayo hayatatuma wanariadha wao maarufu katika michuano hayo katika mashindano yajayo ya mwaka 2018 jijini Lagos nchini Nigeria, watafungiwa kuwakilisha mataifa yao katika michezo ya kimataifa kama ile ya Olimpiki.

Hatua hii inakuja baada ya Kenya na Ethiopia kutowatuma wanariadha ambao wanashikilia mataji mbalimbali ya dunia, kushiriki katika mashindano hayo.

Wanariadha ambao hawakuenda Afrika Kusini, wanaendelea na mazoezi ya kushiriki katika michezo ya Olimpiki nchini Brazil mwezi Agosti.