EURO 2016 - UFARANSA

Wenyeji watinga robo fainali, leo ni zamu ya Itali na Uingereza

Antoine Griezmann, mchezaji wa Ufaransa akishangilia kwa satili ya aina yake baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi dhidi ya Ireland, 26 Juni 2016.
Antoine Griezmann, mchezaji wa Ufaransa akishangilia kwa satili ya aina yake baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi dhidi ya Ireland, 26 Juni 2016. REUTERS

Michuano ya kombe la Ulaya imeendelea mwishoni mwa juma, ambapo tayari timu 6 zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya mwaka huu inayotimua vumbi nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumamosi timu ya taifa ya Poland ilikuwa ni ya kwanza kukata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali baada ya kuitupa nje kwa njia ya matuta, timu ya taifa ya Uswisi, huku katika mchezo mwingine, Wales wakitinga hatua ya robo fainali kwa kuchomoza na ushindi dhidi ya Ireland Kaskazini.

Ureno wao waliponea chupuchupu kutolewa lakini waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Croatia.

Mchezaji wa Ureno, Christian Ronaldo.
Mchezaji wa Ureno, Christian Ronaldo. 路透社

Siku ya Jumapili timu nyingine tatu zilikata tiketi ya kuingia robo fainali, ambapo wenyeji timu ya taifa ya Ufaransa, walichomoza na ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Ireland kwa kuwafunga mabao 2-1, huku katika mchezo mwingine, Ujerumani mabingwa wa dunia, wakifanya kweli na kutinga kwenye hatua ya robo fainali kwa kishindo, baada ya kuwafunga Slovaki kwa mabo 3-0.

Mchuano wa mwisho kwa siku ya Jumapili, ulizikutanisha timu ya taifa ya Hungary iliyokuwa ikijaribu kusaka nafasi ya kucheza hatua ya robo fainali dhidi ya Ubelgiji, lakini ilijikuta harakati zake zikizimwa vibaya kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0, kwenye mchezo ambao Ubelgiji waliutawala kwa dakika zote 90.

Hii leo mechi za hatua ya 16 bora zitaendelea kupigwa, ambapo kutakuwa na michezo miwili ya kukata na shoka, ambapo timu ya taifa ya Italia itakuwa na kibarua dhidi ya mabingwa mara mbili wa michuano hiyo, timu ya taifa ya Uhispiania.

Mechi hii ambayo ni kama ukumbusho wa fainali ya kombe la mataifa Ulaya ya mwaka 2012 ambapo timu hizi zilikutana na Uhispania kuibuka mabingwa, itakuwa ni mechi ngumu na muhimu kwa timu zote mbili kwani Italia iatataka kulipiza kisasi huku Uhispania ikitaka kutengeneza historia nyingine ya kufika hatua ya fainali.

Mchezaji wa Ufaransa, Antoine Griezmann akifunga bao lake la ushindi
Mchezaji wa Ufaransa, Antoine Griezmann akifunga bao lake la ushindi REUTERS/Max Rossi

Mchezo mwingine wa hatua ya 16 bora utakuwa ni ule kati ya timu ya taifa ya Ufaransa ambayo itakuwa ikipepetana na timu ya taifa ya Iceland, katika mchezo ambao unatazamwa sana na mashabiki wa Uingereza.

Uingereza itahitaji ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufika hatua ya fainali, lakini itahitaji kufanya kazi ya ziada kwani vijana wa Iceland wameonekana kudhamiria kuweka historia kwenye michuano ya mwaka huu.

Tayari kocha mkuu wa Uingereza, Roy Hodgson yuko kwenye shinikizo kubwa toka kwa mashabiki wa timu hiyo ambayo wanasema timu yao inacheza chini ya kiwango na kwamba hawaoni ikifika fainali.